Thursday , 30 March 2023
Habari za Siasa

JPM: Hakuna vya bure

Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Dkt John Magufuli
Spread the love

 

RAIS John Magufuli amewaambia wakazi wa Bahi, Dodoma na Tanzania kwa ujumla kwamba, ‘hakuna vya bure.’ Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Amesema, kila mtua anapaswa kufanya kazi na kwamba, katika utawala wake, anataka kila mtu afanye kazi kwani si kazi ya serikali kumlisha mtu.

“Ninawaomba watanzani zangu wa Bahi tuchape kazi, vya bure havipo,” amesema Rais Magufuli akiwa Bahi kuelekea Dodoma akitokea katika ziara mkoani Shinyanga leo tarehe 31 Januari 2021.

Akizungumzia kilimo cha mahindi na tabia ya uvivu kwa baadhi ya wakazi wa Bahi, amehoji inawezekanaje shambo moja likalimwa halafu lingine likawa na pori?

“Haiwezekani mwingine amewivisha mahindi yameweka mbelewele halafu shamba la mtu anayefuata naye hajalima chochote, kuna majani. Hiyo haikubaliki.

“Tunataka hii fedha tunayoitapa ikafanye miradi mkubwa. Tunajenga reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma mpaka Maktupora. Tukimaliza tunataka tuiunganishe hii reli kutoka Maktupora, Tabora mpaka iende Mwanza na iende Kigoma, hiyo ndio kazi ya serikali,” amesema.

Na kwamba, serikali inajenga hospitali, inanunua ndege na inatengeneza barabara kwa sabaubu ndio kazi yake.

“Tunajenga hosptali hiyo ndio kazi ya seikali, tunanunua ndege hiyo ndio kazi ya serikali, tunatengeneza barabara hiyo ndio kazi ya serikali.

“Tunaleta madawa kwenye hospitali ndio maana bajeti tumeiongeza … lakini kukulisha ni kazi yako. Ninawaomba, vyabure havipo,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!