October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

JPM: Hakuna cha bure

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS John Magufuli, ametoa siku 14 kwa taasisi za serikali na binafsi, zinazodaiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kulipa madeni yao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Ametoa agizo hilo leo Jumatano tarehe 22 Julai 2020, wakati akizindua Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jijini Dodoma.

Kiongozi huyo wa nchi amesema, taasisi hizo zinapaswa kuilipa JKT kiasi cha Sh. 11 bilioni, inazodaiwa.

“Ndani ya wiki mbili, taasisi zote zinazodaiwa iwe ofisi ya mkoa, Ikulu, Wizara ya Fedha, Ofisi ya Spika, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais, ndani ya wiki mbili hizi Sh. 11 bilioni zilipwe JKT. Huwezi kuwa unalindwa halafu hulipi,” ameagiza Rais Magufuli.

Pia ameagiza uongozi wa JKT kumpa mrejesho wa taasisi zilizotekeleza agizo hilo.

“Sababu urais bado nitakua nao, wewe nijulishe mahali popote, nijulishe taasisi gani imekataa kulipa hizi fedha, hizi fedha lazima zipatikane sababu hakuna cha bure, taasisi zote zinazohusika za serikali na binafsi mhakikishe mmelipa deni,” amesema Rais Magufuli.

Kuhusu uzinduzi wa ofisi za NEC, Rais Magufuli amemuagiza Jaji Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa NEC kuzihamisha samani za tume hiyo kutoka Ofisi za zamani zilizoko  Dar es Salaam, kwenda katika ofisi mpya Dodoma.

“Vifaa vya Dar es Salaam mvilete hapa msianze na vipya, viwekwe vifaa, vipya vitaharibu taarifa zenu, nikuombe Jaji Kaijage vile viti vyako vya kule Dar es Salaa

error: Content is protected !!