October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

JPM awaweka njia panda Dk. Kigangwalla, Prof. Mkenda

Spread the love

RAIS John Magufuli ametoa siku tano kwa Dk. Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Maliasili na Utalii na Prof. Adolf Mkenda, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, kuondoa tofauti zao vingenevyo ‘atawatumbua’. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 31 Desemba 2019, wakati akizungumza na Maafisa na Askari wa Wanyamapori wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo ….

Kiongozi huyo wa nchi amesema mahusiano mabaya ya  Dk. Kigwangalla na Prof. Mkenda yanasababisha baadhi ya shughuli za wizara hiyo, kukwama.

“Nnafahamu watendaji wenu wa juu Katibu Mkuu wa Wizara kila siku wanagombana, na ninawatazama taratibu. Nilishampa kazi Katibu Mkuu Kiongzi awaite, awaeleze lakini wasipobadilika nitawaondoa. Hilo ni lazima nizungumze kwa dhati,” ameagiza Rais Magufuli na kuongeza;

“Siwezi kuwa na watendaji wa kuteua mimi halafu kila siku wanagombana, kuna mambo mengi hayaendi. Katibu Mkuu hamheshimu Waziri n Waziri nae hataki kwenda na Katibu Mkuu, siwezi kuvumilia hilo.”

error: Content is protected !!