March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

DC, RC wamkera Rais Magufuli

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS John Magufuli amevunja ukimya kuhusu vitendo vya baadhi ya wakuu wa wilaya na mikoa kuwaweka rumande raia. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza katika hafla ya uapisho wa majaji na wakuu wa wilaya wawili Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema kuna masuala mengine yanaweza yakapata ufumbuzi kupitia njia ya mazungumzo kuliko kumweka mtu ndani.

“Wakuu wa wilaya mna mamlaka yenu lakini myatumie vizuri, ni kweli sheria imewapa mamlaka lakini ni muhimu kuyatumia vizuri mamlaka yenu, bahati nzuri hili limeshasemwa sana na watu wengi nami narudia, wakuu wa wilaya mtumie mamlaka yenu vizuri,” amesema Rais Magufuli.

Dk. Magufuli ameeleza kuwa, kumuweka mtu rumande kisha kumtoa pasipo kumpeleka mahakani hakumfanyi mhusika kujifunza.

“Mtu unamweka ndani kisha unamtoa eti amejifunza, amejifunza wapi si ungempeleka hata mahakamani, kuna masuala mengine yanaweza yakaleta athari nzuri kwa maongezi kuliko hata kumweka mtu ndani,” amesema Rais Magufuli.

Kabla ya Rais Magufuli kutoa kauli hiyo, katika mkutano wake na viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali uliofanyika hivi karibuni, Kiongozi wa Kanisa la Efatha, Mtume Josephat Mwingira alimlalamikia kuhusu amri zinazotolewa na baadhi ya wakuu wa wilaya na mikoa kuwaweka watu rumande.

Baadhi ya wakuu wa wilaya waliowahi kutoa amri za kuweka watu ndani ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema aliyetoa amri kwa polisi ya kumkamata na kumuweka ndani diwani wa Kitunda, Nice Gisunte, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi.

 

error: Content is protected !!