Saturday , 10 June 2023
Habari za SiasaTangulizi

JPM aumiza kichwa

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS John Magufuli, ameibua maswali yanayomuumiza kichwa kuhusu tukio la kukamatwa kwa dhahabu ya Tanzania nchini Kenya, bila watuhumiwa kukamatwa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Amehoji, inawezekanaje dhahabu ikapenye kwenye mipaka ya Tanzania, nchi yenye vyombo vya usalama na kisha ikakamatwe na vyombo vya usalama nchini Kenya?

Dhahabu ya Tanzania kiasi cha kilogram 35.34, ilikamatwa na vyombo vya usalama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya mwaka 2018, leo tarehe 24 Julai 2019 imekabidhiwa kwa Rais Magufuli.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya dhahabu hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam Rais Magufuli amehoji “unaweza ukajiuliza maswali mengi, na haya niulize bila kuficha. Ilipokuwa ikibebwa kutoka Mwanza hadi Kilimanjaro, vyombo vya ulinzi na usalama vilikuwa vinafanya nini?

“Je, vilishirikiana na muhalifu au vilimuachia, je dhahabu ngapi zimesafirishwa bila watuhumiwa kushikwa?”

Amesema, dhahabu hiyo imerejeshwa Tanzania, baada ya kuzungumza na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta wilayani Chato hivi karibuni, kuhusu kuachiwa kwa madini hayo na fedha zilizokamatwa nchini humo.

“Serikali ya Kenya ilikamata dhahabu ikisafirishwa mikononi mwa raia wa Tanzania, alipowasili uwanja wa ndege kabla ya kuelekea Dubai. Baada ya kukamatwa, kupitia mikataba ya ushirikiano wa makosa wa jinai, Tanzania na Kenya ilianza kufanya kazi zao. Ninashukuru sana kwa kazi kubwa waliyofanya, ninamshukuru sana ndugu yangu Kenyatta,” amesema Rais Magufuli na kuongeza:

 “Tulizungumza masuala mengi kuhusu mshikamano na ushirikiano ndani ya nchi hizi mbili, nikamuomba ndugu yangu kuna pesa zimekaa huko tangu mwaka 2004 leo ni miaka 15. Lakini pia kuna dhahabu yetu mlikamata huko, akaniambia mwezi wa saba hautapita, dhahabu na mali hizo za Watanzania zitakuwa zimerudishwa.”

Aidha, Rais Magufuli ameahidi kutoa zawadi kwa maofisa waliofanikisha ukamatwaji wa dhahabu hiyo, huku akitoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini Kenya kushirikiana na vya Tanzania katika kutokomeza matukio kama hayo.

Biswalo Mganga, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) amesema, Baraka Chaulo, Raia wa Tanzania alikamatwa na dhahabu hiyo na vyombo vya ulinzi na usalama nchini Kenya mwaka 2018.

“Dhahabu ya kiasi cha Kg. 35.34 ilikamatwa Uwanja wa Ndege Jomo Kenyatta wakati Baraka Chaulo alikuwa anasafiri na ndege ya Precision kutokea Mwanza.

“Ndege hiyo ilitua Kilimanjaro, ikaenda Nairobi ikakamatwa. Nashukuru, tulipofika tuliongea zaidi na DPP wa Kenya kuhakikisha kwamba zoezi hili linafanikiwa,”amesema Mganga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

MichezoTangulizi

Benki ya NBC yakabidhi kombe la ubingwa wa ligi kuu kwa Yanga

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa ligi ya NBC, Benki ya Taifa ya...

BiasharaTangulizi

TLS wajitosa sakata la ukodishaji wa bandari

Spread the love  CHAMA cha wanasheria Tanzania (TLS), kimejitosa katika sakata la...

BiasharaTangulizi

Ngoma bado mbichi mkataba wa Bandari

Spread the love  SAKATA la mkataba wa uendeshaji, uendelezaji na uboreshaji wa...

BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mkataba unaweza kuvunjwa

Spread the loveMKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),...

error: Content is protected !!