December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

JPM ateuwa wenyeviti wapya wa bodi TTCL, Airtel Tanzania

Dk. Omary Nundu, Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Airtel Tanzania (kulia) na Mohamed Mtonga, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Tanzania

Spread the love

DAKTARI John Magufuli ameteua wenyeviti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Bodi ya Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania. AnaripotI Regina Mkonde … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 12 Juni 2019 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa, Rais Magufuli amemteua Mohammed Mtonga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, huku Dk. Omari Nundu akimteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Mtonga anachukua nafasi ya Dk. Nundu aliyeteuliwa kuwa kiongozi wa Bodi ya Airtel.

Sehemu ya taarifa hiyo imefafanua kuwa, uteuzi huo wa Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania umefanyika kufuatia makubaliano yaliyofikiwa kati ya serikali na Kampuni ya Bharti Airtel International kwamba, Tanzania itateua mwenyekiti wa bodi ya kampuni hiyo.

Kufuatia makubaliano hayo, Rais Magufuli amemteua Dk. Prosper Mafole kuwa Afisa Mkuu wa Ufundi wa Airtel Tanzania.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amewateua, John Sausi na Lekinyi Mollel kuwa wajumbe wanaoiwakilisha serikali katika Bodi ya Airtell Tanzania.

“Uteuzi huu unaanza leo tarehe 12 Juni 2019,” inaeleza sehemu ya taarifa ya Msigwa.

error: Content is protected !!