December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

JPM ateua bosi taasisi ya utafiti madini

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS John Magufuli, amemteua Dk. Mussa Budeba, kuwa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST). Anaripoti Faki Sosi … (endelea)

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, uteuzi wa Dk. Budeba umeanza tarehe 15 Novemba 2019.

“Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa, uteuzi wa Dk. Budeba umeanza leo (jana) tarehe 15 Novemba 2019,” inaeleza taarifa ya Msigwa aliyoitoa jana.

Kabla ya uteuzi huo, Dk. Budeba alikuwa Mhadhiri wa Idara ya Uhandisi wa Kemikali na Madini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

error: Content is protected !!