Saturday , 3 June 2023
Home Gazeti Tangulizi JPM atembelea majeruhi, serikali kubeba gharama zote
Tangulizi

JPM atembelea majeruhi, serikali kubeba gharama zote

Spread the love

RAIS John Magufuli amewajulia hali majeruhi 43 wa ajali ya mlipuko wa lori la mafuta iliyotokea mkoani Morogoro, waliohamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakitokea Hospitali ya Rufaa ya Morogoro. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Leo tarehe 11 Agosti 2019 Rais Magufuli ametembelea wagonjwa hao ambao wengi wao wamelazwa katika wodi ya Mwaisela na wengine 8 wamelazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi kwenye hospitali hiyo.

Akizungumza katika tukio hilo, Rais Magufuli amesema serikali itagharamia gharama za matibabu ya majeruhi wote, huku akitoa kiasi cha Sh. 3 milioni kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ya majeruhi hao pamoja na madaktari na wauguzi wanaowapatia matibabu.

“Ninyi endeleji kuwatibu, serikali itagharamia matibabu yote. Bili itakapokuja iletwe serikalini.

Natoa Milioni moja iwasaidie wagonjwa na milioni moja nyingine iwasaidie madaktari na manesi. Tunawaongezea milioni moja nyingine ili wagonjwa na nyie msikose mahitaji. Sijawahonga ila nimewapa iwasaidie wagonjwa,” amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amewataka Watanzania kuwaombea majeruhi wapone haraka, badala ya kuwashushia lawama ya kwamba wameponzwa na wizi wa mafuta.

“Tuendelee kuwaombea huu si wakati wa kuwalaumu, baadhi wanazungumzia hawa wamekwenda kuiba mafuta. Niwaombe sana Watanzania tusiwe na majibu ya haraka hii ni kazi ya Mungu,” amesema Rais Magufuli na kuongeza.

” Sisi tusiwe majaji sababu si kila walioenda walikwenda kuiba mafuta wako walienda kuwaokoa, wwngine walipita njia hafla mlipuko ukatokea.”

Profesa Lawrence Maseru, Mkurugenzi wa MNH amesema hospitali hiyo mpaka sasa imepokea majeruhi 46 ambapo watatu kati yao isivyobahati walipoteza maisha, huku wengine nane wakiwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi.

“Tumepokea wagonjwa 46 walioonekana hawezi kutibiwa Morogoro kutokana na kutokuwepo vifaa. Kwa bahati mbaya watatu wamefariki. Nane wako chumba cha wagonjwa mahututi wanapumua kwa mashine. Wagonjwa wengi sana wameungua sehemu kubwa ya mwili zaidi ya asilimia 70 hadi 80 na wengine zaidi ya 100,” amesema Prof. Maseru.

Naye Dk. Juma Mfinanga, Mkuu wa Kitengo cha Dharula wa MNH amesema majeruhi 15 wamebaki katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro wakiendelea na matibabu.

Dk. Mfinanga ameeleza kuwa, asilimia kubwa ya majeruhi hao ni vijana wenye umri kuanzia miaka 20 hadi 30.

Dk. Elisha Osati, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) amesema wameomba msaada wa madaktari na wauguzi kutoka hospitali nyengine kwa ajili ya kuwahudumia majeruhi hao. Ambapo Jeshi limeahidi kutoa waguzi 60.

“Tumeomba wafanyakazi kutoka jeshi wamesema watatupa wauguzi 60. Na wengine tutawachukua Wananfunzi wa unesi kutoka  MUHAS. Sehemu zote tunafanya kazi siku nzima kuhakikisha wanafungwa vidonda. Tunapambana,” amesema Dk. Osati.

Dk. Osati amesema madaktari na wauguzi wanaendelea kupambana ili kuhakikisha majeruhi hao wanapona upesi kwa uwezo wa Mungu.

” Majeruhi 46 tumewachukua kuwaleta hapa. Watatu bahati mbaya wefariki. Katika chumba cha dharula walikuwa 3, ICU 10 na hapa wodini 33. Hali zao wengi walikuwa wamepata majeraha kwa asilimia 80. Sisin kama watalalum tutafanya wapone mengine Mungu atawaponya,” amesema Dk. Osati.

Ajali ya mlipuko wa tenki la lori la mafuta ilitokea jana tarehe 10 Agosti 2019 majira ya saa 2 asubuhi maeneo ya Msamvu mkoani Morogoro, ambayo imepoteza maisha ya Watanzania zaidi ya 60 na kuacha majeruhi 58.

Katika majeruhi hao, 43 wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na wengine 15 wanatibiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Morogoro.

Leo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine wa kitaifa waliongoza shughuli ya kutambua na kuaga miili ya waliopoteza maisha kwenye mkasa huo.

Taarifa ya serikali inaeleza kuwa, baadhi ya miili itaanza kuzikwa jioni ya leo hadi pale zoezi hilo litakapokamilika.

Pia, serikali imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia jana hadi kesho tarehe 12 Agosti 2019.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!