October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

JPM atangaza siku 7 za maombolezo, bendera nusu mlingoti

Marehemu Benjamin Mkapa

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli ametangaza siku saba za maombolezo kufuatia kifo cha Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa nchi hiyo, Benjamini William Mkapa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema, maombolezo hayo yataanza leo Ijumaa tarehe 24 Julai 2020.

Rais Magufuli amesema, katika kipindi hicho cha siku saba, bendera zote zitapepea nusu mlingoti.

Rais mstaafu Mkapa aliyeongoza Taifa hilo lililopo Afrika Mashariki kati ya mwaka 1995 hadi 2005, amefariki usiku wa kuamkia leo Ijumaa hospitalini jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

error: Content is protected !!