October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

JPM: Asante sana Dk. Shein

Rais wa Tanzania, John Magufuli akiwa na Rais wa mstaafu wa Zanzibar Ali Mohamed Shein

Spread the love

RAIS John Magufuli amemshukuru Dk. Ali Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), anayemaliza muda wake kwa ushirikiano aliompa katika utekelezaji wa majukumu yake. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwa mujibu wa Katiba ya nchi, Rais Shein anamaliza muda wake wa kuiongoza SMZ, katika vipindi viwili mfululizo kuanzia mwaka 2010-2015 na 2015-2020.

Leo Jumanne tarehe 16 Juni 2020 wakati akifunga bunge la 11, Rais Magufuli amempongeza Shein kwa utendaji wake uliotukuka, tangu alipokuwa makamu wa rais wa Zanzibar na Rais.

“Natambua Dk. Shein anamaliza muhula wake kwa mujibu wa Katiba, hivyo nampongeza kwa utumishi uliotukuka akiwa makamu wa rais kwa miaka minane na rais kwa miaka kumi. Rais Dk. Shein kazi umeifanya. Umeweka historia na namna yake katika utumishi wa umma,” amesema Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amewashukuru viongozi waandamizi wa Serikali yake, kwa uwajibikaji wao.

Amewashukuru, Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais na Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu na viongozi wengine.

error: Content is protected !!