Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa JPM asaka wawekezaji Urusi
Habari za Siasa

JPM asaka wawekezaji Urusi

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS John Magufuli amemkaribisha Rais wa Urusi, Vladmir Putin  na wawekezaji kutoka nchi hiyo, kuja kutembelea Tanzania pamoja na kutafuta fursa mbalimbali za uwekezaji zilizoko nchini. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Rais Magufuli ametoa wito huo jana tarehe 13 Machi 2019 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na ujumbe wa Urusi ulioongozwa na Mjumbe Maalum wa Rais Putin katika masuala ya Afrika, Mikhail Bogdanov.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, Rais Magufuli amemuomba Bogdanov ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Urusi,  kumfikishia ujumbe Rais Putin, kwamba serikali anayoiongoza inatambua umuhimu wa uhusiano uliopo baina ya mataifa hayo mawili.

Rais Magufuli amemhakikishia Rais Putin kuwa atauendeleza na kuukuza uhusiano huo, hususani katika masuala ya biashara, uwekezaji, utalii na utoaji wa huduma za kijamii.

“Naomba ufikishe ujumbe wangu kwa Mhe. Rais Putin kuwa watanzania wanaipenda Urusi na tunamkaribisha kuja kutembelea nchi yetu pamoja na wananchi wa Urusi, pia tunawakaribisha wawekezaji waje kuwekeza katika fursa mbalimbali zilizopo Tanzania kwa manufaa yetu sote,” amesema Rais Magufuli.

Naye Bogdanov amemhakikishia Rais Magufuli kwamba Urusi ina mpango wa kushirikiana na nchi za Afrika ikiwemo Tanzania katika kuongeza kasi ya maendeleo, na kwamba hivi karibuni nchi yake pamoja na Tanzania, zitasaini makubaliano ya kuanzisha tume ya pamoja ya ushirikiano katika biashara, uwekezaji na uchumi ili rasilimali na fursa zilizopo kutoka pande zote zitumike kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, amesema mazungumzo kuhusu makubaliano hayo yanaendelea vizuri hivyo Tanzania inatarajia kupata tume ya pamoja ya ushirikiano kati yake na Urusi, itakayosaidia kukuza uchumi kupiutia sekta ya amdini, gesi na utalii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!