September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

JPM apanga matumizi mabilioni ya wahujumu uchumi 

Spread the love

RAIS John Magufuli, ameanza kupanga matumizi ya mabilioni ya fedha zinazorudishwa na watuhumiwa wa uhujumu uchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza katika ziara yake mkoani Katavi leo tarehe 9 Oktoba 2019, Rais Magufuli amesema kiasi cha fedha hizo, zitatumika katika kujenga barabara za kiwango cha lami mkoani humo.

Rais Magufuli ameeleza kuwa, kazi ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuboresha miundombinu hasa ya barabara, na kuwa fedha za kutekeleza kazi hiyo zipo, ikiwemo zile zinazorudishwa na mafisadi.

“Hela zipo, mafisadi wanarudisha hela, tutaacha kumalizia hapa? Lazima tumalize, hizo fedha zinazokuja hizo, zimeanza kuingia huko, wanarudisha mafisadi. Zingine tutazileta hapa kidogo zinatengeneza barabara. Hii ndio kazi ya awamu ya tano,” amesema Rais Magufuli.

Hivi karibuni watuhumiwa wa uhujumu uchumi 467 waliomba msamaha na kuahidi kurejesha zaidi ya Sh. 107 bilioni fedha walizotafuna.

Watuhumiwa hao waliomba toba kufuatia ushauri wa Rais Magufuli, wa kuwataka kukiri makosa, kuomba msamaha kisha kurejesha fedha wanazotuhumiwa kuihujumu serikali.

Mchakato huo unasimamiwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa kushirikiana na mahakama.

error: Content is protected !!