October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

JPM amtumbua mwingine

Rais John Magufuli

Spread the love

WAKILI Julius Kalolo, ameteuliwa na Rais John Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa jana tarehe 17 Juni 2019 na Mkurugenzi wa Mawasiliani ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa.

Taarifa ya Msigwa inaeleza kuwa, uteuzi wa Wakili Kalolo umeanza rasmi jana.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kwamba uteuzi wa Wakili Kalolo umefuatia hatua ya Rais Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya REA, Michael Nyagoga.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Bw. Michael Pius Nyagoga kuanzia leo (jana) tarehe 17 Juni, 2019,” imeeleza taarifa ya Msigwa.

error: Content is protected !!