March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

JPM amteua waziri wa Kikwete

Gregory Teu

Spread the love

RAIS wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania amemteua aliyekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara katika Serikali ya Awamu ya Nne ya Jakaya Kikwete, Gregory Teu kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Kilimanjaro Airport (KADCO), anaandika Faki Sosi.

Taarifa ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliono, Leornard Chamuriho imeeleza kuwa awali Rais Magufuli ametengua uteuzi kwa Balozi Hassan Gumbo Kibelloh kwenye nafasi hiyo na kumchagua Teu kuziba pengo la nafasi hiyo.

Wakati huo huo, Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametengua uteuzi wa Mjumbe wa bodi hiyo bwana Suleiman Suleiman kuanzia tarehe 16 Oktoba.

error: Content is protected !!