April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

JPM ampa Dk. Abbas vyeo viwili

Spread the love

DAKTARI Hassan Abbasi, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ataendelea kutumikia cheo chake cha awali cha Msemaji Mkuu wa Serikali, hadi atakapopatikana mwingine wa kushika nafasi hiyo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Rais John Magufuli leo tarehe 3 Februari 2020, Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati akimuapisha Dk. Abbasi na viongozi wengine wa wizara, aliowateua hivi karibuni.

Rais Magufuli amesema, Dk. Abbasi ametekeleza majukumu yake vizuri katika kuisemea serikali, pamoja na kuzingatia maelekezo ya viongozi wake, akiwemo Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari.

“Amefanya kazi nzuri kama msemaji wa serikali, hakuchoka aliisemea vizuri serikali. Alifuata muongozo mzuri wa Dk. Mwakyembe n a viongozi wengine wa wizara. Tungependa aendelee kuwa msemaji lakini inapotokea mtu apate promotion, usimnyime. Ataendelea kuwa msemaji hadi tutakapopata mwingine,” ameeleza Rais Magufuli.

Pamoja na Dk. Abbasi, Rais Magufuli amewaapisha makatibu wakuu 4 wa wizara,akiwemo Mary Makondo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi. Na makatibu tawala 3.

Wengine walioapishwa ni Brigedia Jenerali Suleiman Mzee, Kamishna Jenerali wa Magereza na Naibu Kamishna wa Magereza, John Masunga, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

error: Content is protected !!