Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM akemea ubaguzi Z’bar, awatumia salamu wapinzani
Habari za Siasa

JPM akemea ubaguzi Z’bar, awatumia salamu wapinzani

Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo akimkabidhi fomu ya kugombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad
Spread the love

RAIS John Pombe Magufuli, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ametuma salamu kwa vyama vya siasa vya upinzani, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Pia, Rais Magufuli amekea vitendo vya kibaguzi Zanzibar kuwa havina tija kwa mustakabari wa visiwa hivyo na kuwataka kuungana na kuwa kitu kimoja.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa CCM jijini Dodoma, leo Jumamosi tarehe 11 Julai 2020, Rais Magufuli amewata wapinzani kuwa wastaarabu katika mchakato wa uchaguzi huo hadi siku ya kupiga kura.

Magufuli amethibitishwa lwa asilimia 100 na mkutano mkuu huo kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia, Dk. Hussein Ali Mwinyi naye amethibitishwa na mkutano huo kuwa mgombea urais wa Zanzibar.

“Napenda kuwathibitishia viongozi wa vyama mbalimbali mimi na Dk. Mwinyi tutashirikiana na ninyi na tutaomba wakati wa kampeni najua mnaelewa kwamba hamtashinda, lakini kuna mahali tutaendelea kuwa pamoja,” amesema Rais Magufuli.

Huku akishanmgiliwa, Rais Magufuli amevitaka vya vya siasa vya upinzani, kutotumia lugha za matusi katika majukwa ya kampeni.

“Kwenye majukwa tusitukanane, tufanye kampeni za kistaarabu wapiga kura wetu wataamua, nawapongeza asilimia 90 ya vyama vinafanya mambo yao kistaarabu kasoro vichache, “ amesema Rais Magufuli.

Mwenyekiti huyo wa CCM, amewataka wanasiasa wa upinzani kuridhika na nafasi walizo nazo, hasa wale wanaogombea katika kila uchaguzi.

“Madaraka haya huwa yanapumbaza na ndio maana inatakiwa viongozi hasa wa vyama inapofika mahali turidhike lakini tujue Mungu hakukuumba wewe tu.”

“Kwa hiyo, nawapongeza sana viongozi wa siasa ambao huwa wanafika mahali wanawaachia wengine kuendeleza kugurudumu la maendeleo,” amesema Rais Magufuli.

Amesema inatakiwa vyama vya siasa viungane kwa ajili ya kulijenga taifa lenye maendeleo, mshikamano na upendo.

Kuhusu uchaguzi wa Urais Zanzibar, Rais Magufuli amewataka WanaCCM kumuunga mkono Mgombea wao, Dk. Hussein Mwinyi na kuacha ubaguzi.

“Niwaombe ndugu zangu wa Zanzibar, achaneni na mambo ya Upemba, Unguja Kaskazini, chukueni Zanzibar moja kwa ajili ya maendeleo ya Wazanzibar mtafanikiwa,” amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amesema, Wazanzibar watapata kiongozi bora na mafanikio kama watamchagua Dk. Mwinyi kuwa rais wao, katika uchaguzi huo.

“Dk. Mwinyi amesimamia kuilinda nchi hii, amesimamia mabomu, mizinga hajaitumia vibaya leo asiende kutawala Zanzibar? Nataka kuwaambia na hili nasema kwa dhati sio mpole ana hekima na unyenyekevu mkubwa, anajua kutunza moyo wake.”

Amesema kama Dk. Mwinyi atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar, atamsaidia kwa nguvu zake zote.

“Na mimi nitamsaidia kwa nguvu zangu zote sababu najua ni mdogo wangu, nataka kuwathibitishia Wazanzibar hamjakosea, ni mneyeneyeku sana, lakini naamini kama atachaguliwa Mwinyi mtayaona matokeo,” amesema Rais Magufuli.

Katika uchaguzi huo, Dk. Mwinyi anatarajiwa kukutana na upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa urais wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif.

Maalim Seif amekuwa akitoa mchuano mkali karibu kila uchaguzi unapofanyika tangu alipoanza kugombea nafasi hiyo mwaka 1995, 2000,2005,2010 na 2015 akiwa Chama Cha Wananchi (CUF).

Mwaka huu, atagombea akiwa ACT-Wazalendo baada ya kujiunga nacho akitokea CUF.

Rais Magufuli amewataka watia nia watakaoanguka katika zoezi la uteuzi wa wagombea wa CCM katika nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani, kutoanzisha mifarakano kwa kuwa ni kikwazo cha ushindi.

Mwenyekiti huyo wa CCM amesema, chama hicho kinapoteza majimbo mengi kwa sababau ya mifarakano.

“Uchaguzi utakapomalizika wa kuteua ndani ya chama chetu, tukaujenge umoja, ni mara nyingi sisi CCM, huwa tunapoteza majimbo sababu ya mifarakano ndani mwetu, anachaguliwa mbunge ambaye hamkutaka na baadae mnajikuta wote mmezikosa hizo nafasi,” amesema Rais Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!