Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo JPM akabidhiwa ramani ya Uwanja
Michezo

JPM akabidhiwa ramani ya Uwanja

Spread the love

RAIS wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na balozi wa Morrocco nchini Tanzania Abdelillah Benry pamoja na waataalam wa ujenzi wa uwanja unaotarajiwa kujengwa Dodoma wenye ukubwa wa kubeba watazamaji elfu 85000. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea)

Katika mazungumzo hayo Rais Magufuli aliweza kuoneshwa ramani ya uwanja huo ambao unaonekana wa kisasa ambao utakuwa ukitumika kwa michezo mbali mbali ikiweno mpira wa miguu, riadha na michezo mingine.

Baada ya mazungumzo hayo balozi wa Morrocco nchini Tanzania amesema kuwa kwa sasa Tanzania na Morrocco wapo katika mazungumzo ya utekelezaji wa miradi mikubwa miwili ambao ni kujenga msikiti na uwanja wa mpira.

“tumekuwa na mazungumzo kuhusiana na mipango ya maendeleo kati ya Morocco na Tanzania. Kwa sasa tuna miradi mikubwa miwili tunaisimamia, ambayo ni ujenzi wa msikiti pamoja na uzinduaji wa ujenzi wa Uwanja wa Soka”, alisema balozi Benry.

Uwanja huo ambao umetengewa hekari 143 unatarajiwa kujengwa eneo la Nara jijini Dodoma ambapo utaghalimu shilingi 56 bilioni sambamba na kituo cha michezo kitakachokuwa kilomita chache kutoka uwanja huo.

Tazama video ya makabidhiano ya ramani hiyo

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Michezo

TFF, Amrouche ngoma nzito

Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...

error: Content is protected !!