Saturday , 22 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM ajibu kombora la Mchungaji KKKT
Habari za SiasaTangulizi

JPM ajibu kombora la Mchungaji KKKT

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS John Magufuli amejibu hoja iliyoibuliwa na Amani Lyimo, Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwamba, ‘amebana’ demokrasia nchini. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Amesema, kuna demokrasia ya kutosha na kwamba, hatoruhusu demokrasia ya matusi jambo ambalo linarudisha maendeleo ya nchini.

Akizungumza na viongozi wa dini mbalimbali kwenye kikao alichokiitisha leo Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema, demokrasia sio kuwepo kwa maandamano.

“…demokrasia ipo ya hali ya juu, kuwepo kwa maandamano sio kielelezo cha demokrasia. Wengine wanatengeneza barabara wengine wanapita na maandamano,” amesema Rais Magufuli.

Amesema kuwa, demokrasia ina mipaka yake na kuwa, hata nchi za nje baada ya uchaguzi, kinachofuata ni suala la maendeleo na si maandamano.

“Demokrasia ina mipaka yake, nyinyi (viongozi wa dini) mmetembea nje sina hakika kama mmeyasikia haya. Mahala tukiendelea kwa utaratibu huu, tutashindwa kujenga nchi,” amesema.

Rais Magufuli amesisitiza kuwa, viongozi wa kisiasa wafanye siasa kwenye maeneo yao ya utawala na si nje ya hapo.

“Hakuna aliyezuiliwa kufanya siasa ndani ya maeneo yao, kilichokatazwa ni mtu kwenda kwenye eneo lingine kutokana,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli alieleza hayo baada ya Mchungaji Lymo alipopata nafasi na kushauri kuwa, alegeze kidogo demokrasia ili Watanzania wapate afueni kutokana na sasa kujaa hofu.

Mbele ya Rais Magufuli, Mchungaji Lyimo amesema, hata kama haambiwi ukweli ni kwamba, Watanzania wana hofu.

“Mhe. Rais, unafanya kazi nzuri sana lakini baba demokrasia, Watanzania wengi wana hofu, hata kama huambiwi na watendaji wako.

“Wengi hawathubutu kuzungumza kwa kuwa wana hofu. Kwa hiyo kama kuna uwezekano baba waachie pumzi kidogo wazungumze,” amesema Mchungaji Lyimo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Padre anayetuhumiwa mauaji ya Asimwe, asimamishwa

Spread the loveKanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha kutoa huduma za kichungaji...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaahidi kushirikiana na Prof. Ndakidemi kuhamasisha zao la kahawa

Spread the loveSerikali imeahidi kuungana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

IMF yaimwagia Tanzania trilioni 2.4 kukabili mabadiliko ya hali ya hewa

Spread the loveShirika la Kimataifa la Fedha (IMF) jana Alhamisi limesema bodi...

Habari za SiasaKimataifa

Mmoja afariki, 30 wajeruhiwa maandamano Kenya

Spread the loveMtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa...

error: Content is protected !!