December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

JPM ‘aingia’ jimboni kwa Lissu

Spread the love

IMECHUKUA siku saba tu kutekelezwa kauli ya Rais John Magufuli, ya kushughulikia tatizo la maji kwenye jimbo la Singida Mashariki lililokuwa likiongozwa na Tundu Lissu. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Miraji Mtaturu, Mbunge wa Singida Mashariki akihojiwa na Redio ya Eat Afrika leo tarehe 23 Septemba 2019, amesema Wizara ya Maji na Umwagiliaji imetoa kiasi cha Sh. 2 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji.

Tarehe 16 Septemba 2019, katika hafla ya uzinduzi wa rada iliyosimikwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), Rais Magufuli alisema, jimbo hilo lilitelekezwa na sasa atalishughulikia.

Kiongozi huyo wa nchi alitoa ahadi hiyo kufuatia ombi la Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa serikali yake, kuhakikisha jimbo hilo linaondokana na changamoto ya uhaba wa maji.

“….Laini pia namuona mheshimiwa wa lililokuwa jimbo limetelekezwa, lilikuwa la Tundu Lissu ameshika huyu. Safi sana, hongereni, mpigieni makofu na ameingia na kazi sababu saa nyingine kwenye majimbo yanakosa uwakilishi,” alisema na kuongeza:

“Na siku ile ulitoa maagizo mheshimiwa spika kwamba, tushughulikie miradi ya maji ya kule kama tulivyoshughulikia Dar es Salaam, nakuahidi tutashughulikia maji katika jimbo lile ili yale yaliyokuwa yamechelewa, yafike harakaharaka.”

Mtaturu ameeleza kuwa, fedha hizo zimetolewa baada ya Jumaa Aweso, Naibu Waziri wa Maji kutembelea jimbo hilo kwa ajili ya kuangalia changamoto zilizopo.

Mbunge huyo wa CCM amesema, serikali imepeleka wataalamu wa maji kwa ajili ya kuangalia namna fedha hizo zitakavyotumika.

“Nashukuru tumepatiwa bilioni 2 na imeleta wataalamu ili kuangalia namna fedha hizo zitakavyogawa kwenye maeneo yenye changamoto za maji,” amesema Mtaturu.

error: Content is protected !!