Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM aagiza mabadiliko ya haraka TAZARA
Habari za Siasa

JPM aagiza mabadiliko ya haraka TAZARA

Spread the love

RAIS John Magufuli ameagiza mchakato wa urekebishaji Sheria ya Reli inayounganisha nchi za Tanzania na Zambia (TAZARA), kufanyika haraka ili kuboresha shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, inaeleza kwamba Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 25 Julai 2019 akiwa safarini kuelekea Kisaki mkoani Morogoro kwa kutumia usafiri wa treni.

Aidha, Rais Magufuli amewaagiza viongozi wa TAZARA kuwasilisha mapendekezo yao juu ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kuboresha usafirishaji wa mizigo na abiria kupitia TAZARA.

“Rais Magufuli ameagiza mchakato wa kufanya marekebisho ya sheria hiyo uharakishwe ili juhudi za kununua injini na mabehewa zifanyike haraka,” inaeleza taarifa ya Msigwa.

Awali Buruno Chingandu, Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA NA Fuad Abdallah, Meneja Mkuu wa TAZARA  Tanzania walimueleza Rais Magufuli kwamba mapendekezo ya mabadiliko ya sheria yamewasilishwa serikalini ili kuwezesha kila nchi kuwekeza katika TAZATA.

Viongozi hao wamesema mapendekezo hayo yana lengo la kuboresha yusafirishaji wa abiria na mizigo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!