Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari JOWUTA, MCT wapongeza Serikali kufungulia magazeti
Habari

JOWUTA, MCT wapongeza Serikali kufungulia magazeti

Spread the love

 

CHAMA cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) na Baraza la Habari Tanzania (MCT), wamepongeza Serikali ya nchi hiyo, kuyafungulia magazeti ya MwanaHALISI, Mawio, Mseto na Tanzania Daima yaliyokuwa yamefungiwa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Taarifa ya kuyafunguliwa magazeti hayo ilitolewa jana Alhamisi, tarehe 10 Februari 2022 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa JOWUTA, Cloud Gwandu alisema uamuzi wa Waziri Nape kutoa leseni kwa magazeti hayo kwa mara nyingine ni wa kupongezwa na kuigwa na watendaji wengine.

“Sisi tunampongeza Waziri Nape kwani ametekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati anazungumza na wahariri mwaka jana, huo ndio uuongozi. Sisi tunaamini kurejeshwa magazeti haya kutasaidia kundi kubwa la waandishi ambalo lipo mtaani bila kazi,” alisema.

Gwandu alisema JOWUTA inapongeza wote waliofanikisha kurejea magazeti hayo, ikiamini kuwa Serikali imeamua kusimamia misngi ya uatawala bora na uhuru wa habari.

“Watoto wa mjini wana msemo wao kuwa Rais Samia anaupiga mwingi, kusema kweli katika hili ameupigwa kweli kweli, lakini pongezi za pekee ziende kwa Waziri Nape na Katibu Mkuu wake, Dk. Jim Yonazi, Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa,” alisema.

Mwenyekiti huyo alisema JOWUTA inaamini uamuzi wa kufungulia magazeti hayo umezingatia misingi ya utu na kuongeza ajira kwa vijana na Watanzania kwa ujumla.

Alisema uamuzi huo umefungua ukurasa mpya kwenye tasnia ya habari, hivyo anawaomba wanaadishi na wamiliki wa vyombo vya habari kuhakikisha wanafuata misingi ya habari ili kuepuka adhabu zisizo na sababu.

Gwandu alisema JOWUTA inapongeza Serikali kuunda kamati ya pamoja kati ya Serikali na wawakilishi wa wanahabari kupitia vifungu vya Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wanahabari na wadau wengine.

Aidha, JOWUTA inaipongeza Serikali kwa kuongeza muda kwa waandishi wa habari kusoma ili kufikia elimu ya Stashahada (Diploma). Uamuzi huu ni muhimu katika kukuza tasnia hii hasa ikizingatiwa hali ambayo imepitia miaka ya hivi karibuni.

Pamoja na pongezi hizo JOWUTA inapenda kuchukua nafasi hii kumuomba Rais Samia na Waziri Nape kuwaagiza wamiliki wa vyombo vya habari kuzingatia sheria ya kazi ambayo inaelekeza wafanyakazi kupewa mikataba ambayo itawezesha kuwepo michango kama ya hifadhi ya jamii, bima ya afya na mingine.

Naye Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, alisema pamoja na pongezi, baraza limepokea kwa furaha ahadi ya Serikali ya kuanza mchakato wa kuzifanyia marekebisho sheria zinazokandamiza uhuru wa habari na wakujieleza.

Kajubi alisema MCT pamoja na wanachama wake 209 linaahidi kushirikiana na Serikali katika maboresho hayo na ni imani yao kuwa yataleta mabadiliko chanya katika kukuza uhuru wa habari na wakujieleza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariHabari Mchanganyiko

CRB yashtukia makandarasi wanaofanya ubia wa ujanja ujanja, yasema watakaobainika kuchukuliwa hatua kali

Spread the love  BODI ya Usajili wa Makandarasi (CRB), imeonya makandarasi wanaofanya...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Habari

Mnyika aacha ujumbe msibani kwa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Taifa, John...

HabariHabari Mchanganyiko

Mwili wa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine wawasili, kuzikwa Mbeya

Spread the loveMWILI wa Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, aliyefia...

error: Content is protected !!