July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jovago yadhibiti wezi wa mitandaoni

Spread the love

KAMPUNI ya Jovago Tanzania imejipanga kuhakikisha fedha za malipo mbalimbali zinazofanywa na wateja wake haziwezi kuibiwa na waharifu wa mitandaoni. Anaandika Erasto Stanslaus … (endelea).

Jovago ni kampuni ya kwanza nchini inayojishughulisha na kuweka oda ya huduma ya mahoteli mbalimbali kwa njia ya mtandao ndani na nje na nchi.

Akizungumza na Mwanahalisi Online, Meneja Uhasibu wa Jovago Tanzania, Charles Wahinya amesema, tatizo la wizi wa mitandaoni limekuwa tishio duniani kote, lakini kampuni yao wamejipanga kuhakikisha fedha za mteja wao zinakuwa salama.

Wahinya amesema kwa upande wao wamehakikisha mteja wao anapotumia huduma ya Jovago kutoa oda ya huduma ya hoteli, fedha zake zitabaki salama, sambamba na taarifa zake za miamala yake inakuwa salama pia.

Jovago tunatumia malipo yetu kwa njia ya tigopesa na Mpesa ambazo haziwezi kuingiliwa na wezi wa mitandao, lakini pia tuna ushirikiano na kampuni ya 3G link ambayo inashughulika na usalama wa miamala ya kwenye mtandano,” amesema Wahinya.

Naye Meneja wa Jovago Tanzania, Andrea Guzzoni amesema ni muhimu kuhakikisha usalama wa fedha za wateja kwenye mitandao, hasa kwa wao wanaofanya bisahara kwa njia ya mitandao.

“Kipaumbele chetu cha kwanza ni kuhakikisha usalama wa fedha za wateja, ndiyo maana Jovago.com imekuwa ni tovuti namba moja Afrika kwa kutoa oda za mahoteli kwa njia ya mtandao,” amesema Gozzoni.

error: Content is protected !!