
Helkopta aliyokuwa amepanda Mbunge, Joshua Nassari baada ya kuanguka
MBUNGE wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amenusurika kifo baada ya ndege aina ya helikopita aliyokuwa amepanda kudondoka akiwa katika ziara katika jimbo lake lilipo mkoani Arusha. Anaandika Pendo Omary … (endelea).
Nassari akiwa na abiria wengine ambao majina yao mpaka sasa hayajapatikana wamekimbizwa katika hospitali ya Seliani, Arusha.
Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene amelithibitishia MwanaHALISI Online kutokea kwa ajali hiyo, huku akiahidi kutoa taarifa kamili muda mfupi ujao.
Endelea kutembelea MwanaHALISI Online itakuleta taarifa kamili ya ajali hiyo juu ya chanzo cha ajali na hali ya Nasarri.
More Stories
ACT-Wazalendo yasema bei ya vyakula imepaa, yatoa mapendekezo
CCM yataka viingilio Sabasaba vipunguzwe
Mahakama yasema uamuzi kesi ya kina Mdee haujakamilika