Tuesday , 27 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Josephat Isango kuzikwa Jumanne
Habari Mchanganyiko

Josephat Isango kuzikwa Jumanne

Josephat isango
Spread the love

MWILI wa aliyekua Mwandishi wa habari Josephat Isango unatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne, saa nne asubuhi nyumbani kwao Kisasida mkoani Singida, anaandika Hamisi Mguta.

Marehemu Isango alifariki dunia jana mapema asubuhi katika hospitali ya Ikungi mkoani Singida ambapo alilazwa kwa wiki mbili akisumbuliwa na Kifua, hata hivyo uchunguzi wa afaya yake ul;ibainisha ana tatizo la kupanuka kwa moyo.

Enzi za uhai wake, Marehemu alifanya kazi katika kampuni mbalimbali ikiwemo Free Media wazalishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari pia aliwahi kufanya kazi katika kampuni ya Hali Halisi Publishers wazalishaji wa magazeti ya Mawio na MwanaHALISI.

Mwandishi huyo ambaye alisifika kwa ujasili wake katika kutetea haki za wanyonge, Mwaka 2015 aliwahi kukumbwa na tukio la kushambuliwa na polisi wa FFU eneo la mbele ya makao makuu ya Jeshi la Polisi katikati ya jijini Dar es Salaam alipokuwa na waandishi wengine wakisubiri kuwasili kwa viongozi wakuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Aliwahi kuugua akiwa jijini Dar es Salaam na baada ya muda mfupi aliamua kusafiri kwenda Singida, mkoa wa nyumbani kwao ndipo mauti yakamkuta.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

Habari Mchanganyiko

Oryx wagawa mitungi 1000 kwa viongozi wa dini, wajasiriamali Moshi

Spread the loveVIONGOZI wa dini kutoka madhehebu mbalimbali pamoja na wajasiriamali katika...

Habari Mchanganyiko

RC Geita awafunda wahitimu wapya GGML

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ametoa wito kwa...

Habari Mchanganyiko

Biteko asisitiza umuhimu wa EREA sekta ya nishati

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!