Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Joseph Selasini: Muongo au msahaulifu?
Makala & Uchambuzi

Joseph Selasini: Muongo au msahaulifu?

Joseph Selasini, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya NCCR Mageuzi
Spread the love

ALIYEKUWA mbunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika jimbo la Rombo, mkoani Kilimanjaro, Joseph Selasini, ameibuka upya na kudai kuwapo mkakati unaosukwa na waliokuwa “marafiki zake,” mimi nikiwamo, kumchafua na kumvunjia hadhi yake mbele ya jamii. Anaandika Saed Kubenea, Dar es Salaam … (endelea).

Anasema, mgogoro wa uongozi unaofukuta ndani ya NCCR- Mageuzi, kwa kiasi kikubwa, unachochewa na hatua ya baadhi yetu, kutumiwa na mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia.

Alisema, “…najua kabisa, najua ndiyo maana namuambia Mbatia, amwambie Kubenea aache, kwa sababu, mimi naweza kutoa ya familia yake, kwa kuwa tunafahamiana. Hata Kubenea, naweza kutoa ya kwake pia. Ninamfahamu. Sisi tumekuwa wote kwa muda mrefu.

“Lakini mimi ni mtu mzima, nakwenda kwa hoja. Mimi siendi kwa mambo ya Kiswahili. Yaani watu wanachukulia vitu kwa mambo ya mtaani, katika mambo mazito. Siyo sahihi kusema kuwa huyu hastahili katika jamii, kwa kuwa ni mhuni, ili nini? Sisi tunaangalia nini analeta, si uhusiano wake,” alieleza.

Msingi wa madai ya Selasini, ni taarifa zinazoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari, zikimnukuu Dk. Masumbuko Lamwai, mmoja wa wanawazuoni mashuhuri nchini, akielezea maisha ya Selasini, mwenendo wake, tabia zake na hulka yake.

Dk. Lamwai, aliyekuwa mhadhiri mwandamizi wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), mbunge wa Ubungo na Mkurugenzi wa Katiba na Sheria (NCCR-Mageuzi), ameeleza mengi kuhusu mwanasiasa huyu.

Aidha, Dk. Lamwai, aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Dar es Salaam, diwani wa kwanza wa upinzani katika Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, kupitia kata ya Manzese na baadaye Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, na Joseph Roman Selasini Shao, ni watoto wa Mzee Roman Selasini na mkewe, Katharine Shao.

(Habari kamili inapatikana katika gazeti la Raia Mwema la leo Ijumaa).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziTangulizi

Askofu Bagonza: Potofu huzaa potoshi/ potoshi huzaa potofu?

Spread the loveDayosisi 7 za KKKT katika kanda ya Ziwa na Magharibi,...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

error: Content is protected !!