May 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Jose Mourinho atimliwa Tottenham

Jose Mourinho

Spread the love

 

TIMU ya Tottenham Hotspur ya Uingereza, imemfukuza kocha wake mkuu, Jose Mourinho kutokana na mwenendo usioridhisha. Anaripoti Matrida Peter … (endelea).

Mourinho ametimliwa leo Jumatatu tarehe 19 Aprili 2021, kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu hiyo ambayo sasa, iko nafasi ya saba ya Ligi Kuu ya Uingereza na pointi 50 kati ya michezo 32 iliyocheza.

Michezo hiyo, ndiyo imechezwa na vinara wa ligi hiyo, Manchester City yenye pointi 74.

Kocha huyo mwenye maneno mengi, alijiunga na timu hiyo, Novemba 2019 na mkataba wake ulikuwa umalizike mwaka 2023. Alichukua nafasi iliyokuwa imeachwa wazi na Mauricio Pochettino ambaye naye alitimliwa.

Vyanzo mbalimbali vya habari, vinawataja makocha Ryan Mason na Chris Powell kwamba wanaweza kurithi mikoba ya Mreno huyo, Mourinho ambaye amewahi kutimliwa Manchester United na Chelsea zote za ligi kuu ya Uingereza.

error: Content is protected !!