Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Jonathan ajitosa Urais Nigeria kupitia chama kilichomng’oa
Kimataifa

Jonathan ajitosa Urais Nigeria kupitia chama kilichomng’oa

Aliyekuwa Rais wa zamani wa Nigeria Gooluck Jonathan
Spread the love

 

ALIYEKUWA Rais wa zamani wa Nigeria Gooluck Jonathan, kupitia chama cha tawala cha People’s Democratic Party (PDP), amejitosa tena kuwania kurejea madarakani katika uchaguzi wa mwaka ujao,kupitia chama cha All Progressive Congress (APC) chama ambacho kilimshinda mwaka 2015, baada ya kukaa madarakani kwa miaka mitano. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa Mashirika ya Kimataifa … (endelea).

Uamuzi aliochukua Goodluck kuingia kwenye kinyang’ anyiro kuwania urais, kupitia chama cha APC umewashangaza sana Wanageria wengi, hasa wale wa chama chake cha zamani People ‘s Democratic Party (PDP), hata hivyo kundi la wafuasi lilinunua fomu ya uteuzi kwa niaba yake siku ya jana jumatatu tarehe 9mei 2022, na kuendeleza mtindo wanaotaka kutumia washirika kununua fomu hiyo.

Hata hivyo kwamuda wa miezi kadhaa, uvumi umekuwa ukizagaa kuhusu kujihusisha kwake kwa siri katika chama tawala lakini Jonathan wala washirika wake ,hawajatoa maoni yao.

Bado haijabainika kwa nini Jonathan aliamua kubadili chama, lakini kumekuwa na fununu kwamba amekuwa hana furaha kutuatia kushindwa kwake kwenye uchaguzi wa mwaka 2015, ambapo inasemekana alihisi kusalitiwa na washiriki wake wakuu ndani ya chama.

Aidha anasema kuwa ‘’ anastahiki muhula mmoja zaidi iwapo atashinda katika uchaguzi wa mwaka ujao,jambo ambalo linaweza kuimarisha mamlaka kurejea katika eneo la Kaskazini mwa Nigeria katika mpangilio ambao haujaandikwa, wenye utata ambao unabadilisha mamlaka kati ya Kaskazini na kusini’’ alisema Jonathan.

Pia akiongeza kuwa yeyote atakayepata uteuzi huo wa APC, atatarajia ushindani mkali kutoka kwa PDP.wagombea wake kama vile Peter Obi,Makamu wa Rais wa zamani Atiku Abubakar na gavana wa jimbo la Rivers Nyesom Wike ni maarufu sana, haswa kusini mwa Nigeria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!