May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jonas Mkude arejea Simba

Spread the love

 

JONAS Mkunde, Kiungo mkabaji wa mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara 2020/21 na kombe la shirikisho, Simba ya jijini Dar es Salaam, amerejea tena ndani ya kikosi hicho, baada ya kusimamishwa kwa utovu wa nidhamu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mkude ambaye amehudumu ndani ya kikosi hicho kwa zaidi ya miaka nane alisimamishwa na uongozi wa Simba, takribani miezi mitatu iliyopita kwa utovu wa nidhamu akituhumiwa kutokuripoti kambini na kutohudhuria mazoezi tarehe 18 Mei 2021.

Baada ya kusimamishwa, kamati ya nidhamu inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Suleiman Kova ilikutana na pande zote mbili kusikiliza tuhuma zilizokuwa zikimkabili mchezaji huyo.

Tarehe 7 Juni 2021, taarifa ya Kova ambaye amewahi kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ilisema, baada ya kusikiliza pande zote, kamati iliiagiza menejimenti ya Simba kwamba Mkude akafanyiwe vipimo vya afya katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.

Ni baada ya kujirudiarudia kwa matendo kama hayo na mchezaji huyo.

Kova alisema, baada ya kufanyiwa vipimo, kamati hiyo itakutana na kutoa uamuzi wa mwisho.

Hata hivyo, hakuna taarifa yoyote iliyotolewa hadi leo Jumatatu tarehe 9 Agosti 2021, ambapo mitandao ya kijamii ya Simba imeweka picha za wachezaji mbalimbali wakiwasili kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22.

Miongoni mwa wachezaji hao ni kiungo wao mkabaji, Jonas Mkude akiwa na wachezaji wenzake wakiwa na nyuso za furaha.

error: Content is protected !!