July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

John Walker afariki dunia

Spread the love

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Dennis Mhina maarufu kama John Walker amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Muhimbili, alipokuwa amelazwa kutokana na kupata ajali ya kuripukiwa na mtungi wa gesi.

Akiongea kwa simu kaka wa Marehemu Omari Milay, amesema walipokea taarifa kutoka hospitali kwa madaktari kuwa mpendwa wao amefariki dunia akiwa akipata matibabu.

John Walker alipata ajali ya kugongwa na kitu kizito kwenye paji la uso, alipokuwa gereji maeneo ya Sinza akitengeneza gari yake, ambapo kwa bahati mbaya mtungi wa gesi ukalipuka na moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani,

Taarifa za awali za madaktari zilisema wanahofia kipande hiko kimefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo.

Mipango ya mazishi familia imesema inakutana kujadili na mara itakapokamilika watajulisha watu nini kinaendelea.

Msanii John Walker ambaye alikuwa kwenye kundi la Watukutu Family, alijipatia umaarufu kwa nyimbo zake za Sophia, Baby gal na nyinginezo, ambazo aliziimba kwa mtindo wa ulevi.

error: Content is protected !!