May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Joe Biden azidi kumuadhibu Trump

Spread the love
RAPHEI Warnock, ndio seneta wa kwanza mweusi katika jimbo la Georgia, nchini Marekani. Anatokea chama cha Democrat cha rais mteule, Joe Biden. Anaripoti Mwandishi Wetu kwa msaada wa mashirika ya kimataifa…(endelea).

Democrat kimenyakua viti viwili katika jimbo la Georgia katika uchaguzi wa marudio uliofanyika jana. Kabla ya uchaguzi huo, viti hivyo, vilikuwa vinashikiliwa na mahasimu wao wa kisiasa – Republican.

Mwingine aliyeibuka kidedea, ni Jon Ossoff; wameibuka washindi dhidi ya Maseneta waliokuwa wakitetea viti vyao, Kelly Loeffler na David Perdue.

Hili ni pigo kubwa la kisiasa kwa rais anayeondoka madarakani, Donald Trump wa Republican.

Kwa mara ya kwanza toka mwaka 2009 chama cha Democrat kitakuwa na udhibiti wa Ikulu ya White House, Bunge la Wawakilishi (Congress) na Bunge la Juu (Seneti).

Takriban watu milioni nne walijitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa marudio jimboni Georgia.

Uchaguzi huo wa Maseneta ulilazimika kurejewa kwa kuwa hakuna aliyefikia asilimia 50 ya kura ulipofanyika uchaguzi mkuu Novemba 2020.

Bwana Warnock, ambaye ni mchungaji wa kanisa la Baptist, anakuwa seneta wa kwanza mweusi wa Georgia, jimbo ambalo liliingia katika vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani ikitaka utumwa uendelee.

Pia anakuwa seneta wa 11 mweusi katika historia ya Marekani.

Jon Ossoff ni mtayarishiji wa makala ya filamu mwenye umri wa miaka 33.

Je, matokeo haya yana maana gani?

Kwanza, matokeo ya Georgia, yanaifanya Democrat na Republican kuwa na viti 50 katika Bunge la Seneti.

Hata hivyo, Makamu wa rais ajaye kutoka Democrat, Kamala Harris, ataongoza wenzake katika Bunge la Seneti na atakuwa na kura ya ushindi kwenye mijadala.

Hali hiyo itaupa uongozi wa Biden nafasi kubwa ya kutekeleza ajenda zake zikiwemo huduma za afya na mabadiliko ya tabianchi.

Seneti pia ina nguvu ya kupitisha ama kuwakataa wateule wa bwana Biden katika nafasi za mawaziri na mahakama.

Pili, ushindani ulikuwa mkubwa katika uchaguzi wa viti vyote viwili.

Mchungaji Warnock amepata asilimia 50.7 dhidi ya asilimia 49.3 alizopata Seneta Kelly Loeffler ambaye ni mfuasi mkubwa wa Trump.

Rais Trump anaendelea kutoa madai yasiyokuwa na ushahidi ya wizi wa kura, huku akitilia mashaka uhalali wa uchaguzi wa Georgia.

Bwana Trump amesikika katika mkanda wa sauti uliovuja siku ya Jumapili akimshinikiza afisa wa juu wa uchaguzi wa jimbo hilo, Brad Raffensperger, ambaye pia ni mwanachama wa Republican, “kutafuta” kura za kutosha ili kupindua ushindi wa Biden katika jimbo hilo.

Je, Maseneta hawa wateule ni akina nani?

Raphael Warnock (51), ni mchungaji katika kabisa la Ebenezer la Baptist jijini Atlanta -kanisa ambalo mpigania haki za watu weusi nchini humo Martin Luther King pia aliwahi kuhudumia.

Bw Warnock alikuwa mchungaji kijana katika jiji la New York miaka ya 1990 kabla ya kuhamia Baltimore, moja ya jiji maskini zaidi nchini Marekani.

Katika jiji hilo alifanya kazi ya kuwaelimisha wafuasi wa kanisa lake juu ya hatari za virusi vya HIV na Ukimwi. Pia ni mtetezi wa utoaji mimba, jambo linalomfanya kuwa miongoni mwa viongozi wachache wa kidini wanaounga mkono jambo hilo na anapinga pia adhabu ya kifo.

Mwaka 2013, aliongoza sala kwenye sherehe ya kuapishwa rais Barack Obama kwa muhula wa pili.

Jon Ossoff, 33, ni mtayarishaji wa filamu kutoka jijini Atlanta. Akiwa mwanafunzi wa sekondari alifanya mafunzo kwa vitendo katika ofisi ya mwakilishi maarufu wa Democrat na mpigania haki za watu weusi John Lewis, ambaye alifariki 2020.

Baadae akiwa msaidizi wake kwenye masuala ya usalama na mambo ya nje.

Mwaka 2012, Bw Ossoff Ali kiungo na kampuni ya utengenezaji wa makala za uandishi wa habari wa uchunguzi, Insight TWI, yenye maskani yake jijini London. Kwa sasa ndiye Afisa Mtendji Mkuu wa kampuni hiyo.

error: Content is protected !!