September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Joao Lourenco aibuka mshindi Angola

Joao Lourenco

Spread the love

CHAMA cha People’s Movement for the Liberation of Angola (MPLA) nchini Angola kimeshinda uchaguzi mkuu uliofanyika jumatano ya wiki hii kwa zaidi ya asilimia 64, anaandika Victoria Chance.

Chama hicho kilicho tawala nchi ya Angola kwa zaidi ya miaka 40 kimeibuka na ushindi kupitia mgombea wake Joao Lourenco (Waziri wa ulinzi nchini) Angola ambaye atapokea madaraka kutoka kwa Eduardo Dos Santos aliyeongoza nchi ya nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 38.

Licha ya Rais Dos Santos kuachia madaraka ataendelea kuwa mwenyekiti wa chama cha People’s Movement for Liberation of Angola.

Rais mpya wa Angola Joao Lourenco atakabiliwa na changamoto zilizoachwa na Rais wa zamani ambazo ni za kiuchumi licha ya kuwa nchi hiyo ni ya pili kwa uzalishaji wa mafuta barani Afrika.

error: Content is protected !!