December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

JKT wakabidhiwa kiwanda cha korosho Lindi

Baadhi ya sehemu ya mtambo ya kiwanda cha Korosho cha Buko, mkoani Lindi

Spread the love

BAADA ya Serikali kukitwaa kiwanda cha kuchakata korosho kilichopo mkoani Lindi Buko, Rais John Magufuli amekikabidhi kiwanda hicho kwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza leo tarehe 12 Novemba 2018 Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema kiwanda hicho kitakuwa chini ya JKT na kwamba endapo jeshi hilo litashindwa kukiendesha, litanyang’anywa na kukabidhiwa kwa watu wengine.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ameagiza korosho zitakazonunuliwa na serikali, kiasi zipelekwe kwenye kiwanda cha Buko.

“Korosho hizo zikinunuliwa jeshi litapeleka kwenye magodauni, hiyo korosho itakayosombwa itapelekwa nyingine kwenye kiwanda cha Buko mkoani Lindi, kiwanda hiki nimewapa wanajeshi JKT mpaka hapo kikiwashinda kukitumia tutawanyang’a, tutakipeleka kwa watu wengine,” amesema Rais Magufuli.

error: Content is protected !!