January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

JK mgeni rasmi vita dawa za kulevya

Rais Jakaya Kikwete

Rais Jakaya Kikwete

Spread the love

RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasm katika siku ya maadhimisho ya kupiga vita dawa za kulevya duniani. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Maadhimisho hayo ambayo kilele chake kitakuwa Juni 26 mwaka huu, yatafanyika katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Hayo yameelezwa kwa waandishi wa habari na Naibu Waziri wa Afya, Dk. Steven Kebwe kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Jenester Muhagama.

Mbali na hali hiyo Dk. Kebwe amesema, kwa sasa inakadiriwa watumiaji wa dawa za kulevya aina ya heroin ni kati ya 200,000 na 425,000.

Dk. Kebwe amesema, tatizo la dawa za kulevya bado ni kubwa nchini ambapo biashara hiyo inaenddelea kuwepo licha ya jitihada kubwa zinazofanywa na serikali.

“Serikali imekuwa ikiwakamata waingizaji na wauzaji wa dawa hizo. Mwaka 2014 jumla ya tani 81 za bangi,16 mirungi kiro 40 za heroin na kilo 45 za kokeini zilikamatwa,” amesema.

Amesema, kuwepo kwa biashara na matumizi ya dawa za kulevya kumeitumbukiza jamii kwenye matukio ya uharifu.

Kutokana na hali hiyo ya kuwepo kwa dawa za kulevya amesema, jamii imejikuta ikiwa na vijana wa tegemezi, kuenea kwa maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) na homa ya ini pamoja na migogoro ya kifamilia.     

Dk. Kamwe amesema, kutokana na kuwepo kwa vijana wengi kujingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya imefikia hatua ya vijana wengi kupoteza akili zao na kusababisha vijana hao kuwa na ugonjwa wa hakili.

error: Content is protected !!