
Rais Jakaya Kikwete akihutubia Bunge
KUTOKANA na hali ilivyo kwa sasa bungeni kuna uwezekano mkubwa wa Rais Jakaya Kikwete akawahutubia wabunge wa Chama kimoja yaani CCM wakati wa kulivunja bunge. Anaandika Dany Tibason … (endelea).
Hali hiyo imejionesha baada ya spika wa Bunge kuwapatia adhabu wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kupinga upitishwaji wa muswada ya mafuta na gesi.
Kutokana na hali hiyo spika alitaa adhabu ya siku tano kwa wabunge hao kwa madai kuwa wamekikosea kiti adabu na kuwapa adhabu ya kutohudhuria vikao hivyo kwa siku tano, siku nne pamoja na siku mbili.
Kizaazaa cha kuwafukuza wabunge wa upinzani kilianza juzi jioni baada ya wabunge 11 kutimuliwa bungeni huku wakiwa wanapatiwa adhabu tofauti.
Hali hiyo hali hiyo iliendelea kufikia hilo ambapo wabunge 35 kutimuliwa bungeni kwa majina na kupewa adhabu ya kutohudhuria vikao vitano ikiwa ni pamoja na wengine kupewa onyo kali.
Pamoja na wabunge wa CCM kubaki peke yao huku miswada hiyo ikiwa imegomewa na wapinzania bado wabunge wa CCM hawakuonesha kiwango cha kujadili na badala yake wamejikita katika kuonesha umairi wao vijembe kwa wapinzani.
Kila mbunge ambaye alipata nafasi ya kuchangia hakuwa na tofauti na mjadala wa Bunge Maalum la Katiba kwani walio wengi badala ya kuchangia mambo ya msingi walikuwa wakirusha vijembe kwa wapinzani.
Hata hivyo bado sinema hiyo inaweza kendelea leo au kesho kutokana na kuongeza siku za kuendelea na shughuli za bunge kwa siku ya jumapilia na katika sikuu ya sabasaba.
More Stories
Ni bajeti yenye neema kwa Watanzania
Joseph Selasini: Muongo au msahaulifu?
Mjue mtunzi; Upande wa pili wa watunzi wa riwaya nchini