July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

JK amnadi Magufuli

Spread the love

RAIS Jakaya Kikwete (CCM) leo amemnadi mgombea Urais kupitia chama hicho John Magufuli katika viwanja vya Jangwani ikiwa ni siku moja kabla ya mgombea huyo kumalizia kampeni zake mjini Mwanza hapo kesho. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Mkutano huo wa kumnadi Magufuli unafanyika zikiwa zimebaki siku mbili kuifikia siku ya kuwaachia wananchi maamuzi nani atakayekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu ya tano.

Kikwete amemnadi mgombea huyo akimsifu kuwa ni mwenye msimamo wa kuhakikisha haki na kujali wanyonge katika matatizo mbalimbali.

Amemsifu Magufuli kuwa ni mtu mwenye maamuzi magumu katika kazi zake na kuwa akiamua kitu ndivyo anavyofanya na kutekeleza kwa maslahi ya wananchi.

Magufuli mwenye kauli mbiu ya ‘hapa kazi tu’ ambaye pia katika hoja zake anaonekana kusisitiza kushikilia na kuzimamia viwanda kuleta maendeleo na kusisitiza kuwa serikali yake itakuwa ya viwanda pindi atakapopata ridhaa ya kuwa Rais.

Kesho Mgombea huyo anatarajiwa kumalizia kampeni zake Jijini Mwanza huku Edward Lowassa mgombea kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), atafanya mkutano wa kufunga kampeni huku Magufuli akimalizia mkoani Mwanza.

error: Content is protected !!