August 12, 2022

Uhuru hauna Mipaka

JK ainanga CCM, amwonya JPM

Spread the love

KUONGOZA Chama Cha Mapinduzi (CCM) si lele mama. Ndivyo anavyosema Dk. Jakaya Kikwete, mwenyekiti wa sasa wa chama hicho, anaandika Dany Tibason.

Na kwamba, chama hicho kilikuwa na ‘mafisi’ wengi waliokuwa wakisubiri ‘mkono’ udondoke kisha wachekelee.

Kauli hiyo inaeleza mnyukano halisi uliokuwepo ndani ya chama hicho wakati wa mchakato wa kumsaka mgombea wa chama hicho katika ngazi ya urais mwaka jana.

Dk. Kikwete ambaye ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne anayemaliza muda wake, amemtahadharisha Dk. John Magufuli, mwenyekiti mtarajiwa wa chama hicho kuwa, uenyekiti wa CCM is lelemama. “Wajumbe wasipoelewa wanachokitaka, wanakuwa wakali sana.”

Dk. Kikwete ametoa kauli hiyo jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa halmashauri kuu ya chama hicho ambapo ajenda alikuwa kujadili na kupitisha jina la mwenyekiti ambalo litapelekwa katika mkutano mkuu utaofanyika leo kwa lengo la kupigiwa kura.

Amesema, Rais Magufuli atakuwa mwenyekiti na kwamba, wakati mwingine kikao huwa kigumu kwani wajumbe hutaka kutendewa haki na wasipopata haki zao, wanakuwa wakali sana.

Amesema, wajumbe wa vikao ni wepesi sana kusifia lakini wanakuwa wakali sana pale ambapo mambo yanaenda vibaya hivyo kiongozi ni lazima kumsikiliza na kujua nini ambacho wajumbe wanataka.

Dk. Kikwete amesema, wajumbe hao wanakuwa wakali kwa kuwa, wanataka mambo ndani ya chama yaende vizuri ili nao ndani ya chama waweze kujivunia.

Kauli hiyo inaelezwa kutafsirika kama tahadhari kwa Rais Magufuli ambaye amekuwa akielezwa kufanya uamuzi katika serikali bila kuzingatia taratibu na kanuni za nchi kwamba, ndani ya CCM asifanye mambo hayo.

Hivi karibuni, ndani na nje ya chama hicho kumekuwa na malalamiko dhidi ya hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Rais Magufuli kwamba zinaumuza nchi na kuwa, ‘washauri wake wanampotosha.’

Hata hivyo Dk. Kikwete amesema, “CCM ilikuwa ivunjike wakati wa kipindi kigumu cha uchaguzi wa mwaka jana lakini tunamshukuru Mungu kwa kuwa tumeweza kukaa imara na kukitafa chama kutovunjika.

“Tunasema kikao kama hiki hatumwi mtoto, tunakuja wenyewe kikao cha leo ni kikao cha kihistoria, kwa namna mbili; kwanza ni kikao changu cha mwisho.

“Nikija kwenye NEC ni pale mtakaponialika lakini tulikubaliana kwamba, wazee hao wameishatumikia vya kutosha na tuwaache wapumzike utaratibu wa hapo nyuma ukimaliza uenyekiti unakuwa mjumbe wa kudumu wa kamati kuu na halmashauri kuu.

“ Siku moja Mzee Mkapa akasema bwana mbona sisi wazee mnatusumbua sana, mnatuhita kila siku na sisi tumeisha kuwa wazee tunakaa mpaka saa saba usiku kwa hivi sasa tuacheni, ndipo niliposema hatuwezi na tukaamua kuunda baraza la wazee.”

Dk. Kikwete amesema, waliona hawawezi kuwahita kila siku “lakini tunawatengenezea baraza la wazee ambalo ni baraza la ushauri. kimsingi linahitajika kwa jambo muhimu sana kama ilivyo kuwa mwaka jana. Nilijadiliwa nikaambiwa JK hataki wazee lakini nikasema huo ni uamuzi wa busara kabisa.

“Kuna maswala mkubwa ya chama chetu na uhai wake kama ilivyokuwa mwaka wa jana, eeee chama chetu kilikuwa kimekaa katika msukosuko mkubwa, mnaingia hapa watu wanaimba hiki wanaimba kile mjadala mkali lakini nikasema tutavuka tu maadamu tupo ndiyo changamoto ya uongozi.

Dk. Kikwete amesema, “maadamu CCM haikuvunjika kama haikuvunjika mwaka wa jana, haitavunjika tena.”

Mbali na hayo amesema, wajumbe wanatakiwa kushirikiana na mwenyekiti mpya ili kukifanya chama kuweza kusonga mbele zaidi.

 

error: Content is protected !!