January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Jitoeni kwa watoto wenye mahitaji’

Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Thami Mseleku

Spread the love

BALOZI wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleku ameyataka mashirika mbalimbali kusaidia watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kumuenzi aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela. Anaandika Hamisi Abdallah na Faki Sosi, DSJ … (endelea).

Aliyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Nelson Mandela katika Hospitali ya taifa Muhimbili (MNH) ikiwa ni sehemu ya kumuenzi.

Maadhimisho hayo ambayo hufanyika julai 18 kila mwaka duniani kote, yaliyohairishwa na kufanyika ili kupisha Sikukuu za Eid Elfitir iliyosherekewa wiki iliyopita baada ya waisilamu kote nchini kumaliza mfungo.

Maadhimisho hayo yaliambatana na ziara ya kutembelea wodi ya watoto wenye matatizo ya kuvimba kichwa (kichwa kujaa maji) iliyohudhuriwa na vijana kutoka shule za sekondari pamoja na taasisi mbalimbali kwa kushirikina na Umoja wa mataifa (UN) kwa lengo la kuwasaidia usafi na kuwapatia mahitaji muhimu kama chakula,vyombo vya kufanyia usafi na nguo.

Akizungumza na MwanaHalisionline,Balozi Mseleku amesema dakika 67 za shughuli hizo zimetokana Nelson Mandela aliejitolea siku 67 kwa kupambana na kutetea haki za binadamu na jamii katika bara la Afrika, hivyo maadhimisho hayo yanasaidia kugundua matatizo mbalimbali ya wagonjwa na kuwapa misaada husika.

error: Content is protected !!