Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Jinsi Magufuli alivyomuaga mama yake
Habari Mchanganyiko

Jinsi Magufuli alivyomuaga mama yake

Spread the love

 

ALIYEKUWA Rais wa Tanzania, Hayati John Pombe Joseph Magufuli (61), alimuaga mama yake Suzan Magufuli, kwa kumuombea sala. Anaripoti Mwandishi Wetu, Chato … (endelea).

Hayo aliyasema Ngusa Samike, Msemaji wa Familia ya Magufuli, jana Ijumaa tarehe 26 Machi 2021, baada ya mwili wa Dk. Magufuli kuzikwa katika makaburi ya familia, kijijini kwao Chato mkoani Geita.

Dk. Magufuli alifariki dunia tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, iliyopo Makumbusho mkoani Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu ya matatizo ya mfumo unaosafirisha umeme kwenye moyo.

Samike alisema, tukio la Hayati Magufuli kumuaga kwa mara ya mwisho mama yake anayeumwa kiharusi kwa zaidi ya miaka miwili, lilifanyika Januari 2021, wakati Magufuli alipokwenda nyumbani kwao Chato.

“Nakumbuka mara ya mwisho alipoondoka nyumbani Chato mwezi Januari, tendo lake la mwisho alikwenda kumuaga mama yake na kisha alisari na kuomba hii ilikuwa ni kawaida lakini pia ni namna alivyoagana na mama yake kwa mara ya mwisho,” alisema Samike.

Msemaji huyo wa familia ambaye pia alikuwa katibu wa Hayati Magufuli alisema, kiongozi huyo alikuwa anapenda kusali na hata kabla ya kufikwa na mauti aliwoangoza madaktari na wauguzi kusali na kuimba.

“Sisi wanafamilia tunamfahmu mpendwa wetu, alipenda sana kusali na kumtanguliza Mungu kwa kila jambo.”

“Alikuwa hawezi kufanya jambo lolote bila kusali, hata akitaka kusafiri ilikuwa lazima afanye sala au maombi, na hata alipofika mwisho wa safari alifanya hivyo hivyo kwa kumshukuru Mungu,” alisema Samike.

Samike alisema, Kardinali Polycarp Kardinali Pengo, kwa kumuongoza Dk. Magufuli katika sala ya mwisho, kabla hajafariki dunia.

“Familia inapenda kutoa shukrani za dhati kwa Kardinali Pengo na Paroko wa Kanisa la St. Perter, Padri Makubi ambaye walimuongoza mpendwa wetu kwa sala na mpako wa mwisho.”

“Tunamshukuru pia Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir, kwa kumuombea dua muda mfupi kabla hajaaga dunia,” alisema Samike.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!