JINAMIZI la kisiasa limezidi kumkalia kooni mwenyekiti wa sasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Mwanza, Antony Diallo baada ya kuibuka tuhuma dhidi yake kwamba ameanza kampeni za kumchafua mgombea mwenzake, Meck Sadik, anaandika Moses Mseti.
Sadik alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro katika utawala wa awamu ya tano ya Rais John Magufuli, lakini aliachia nafasi hiyo kwa madai kwamba ameamua kupumzika.
Diallo anadaiwa kumchafua Sadik kwa kusema kwamba ni pandikizi la aliyekuwa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa.
Mikosi ya kisiasa ilianza kumuandama Diallo tangu mwaka 2010 aliposhindwa nafasi ya ubunge na kiti chake kuchukuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Taarifa zinaeleza kwamba, tangu Diallo ashindwe kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Highness Kiwia (Chadema) ameendelea kuporomoka na ushawishi wake ndani na nje ya mkoa umeshuka.
Hata hivyo tuhuma hizo hazikuthibitishwa kutokana na Diallo kutopatikana kwenye simu zake ili kuzungumzia tuhuma.
Leave a comment