January 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jiji lajivua lawama za wauza samaki Ferry

Mwenyekiti wa Soko la wauza samaki Ferry, Rajabu Mngoi

Spread the love

SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa  Soko la  wauza samaki Ferry, Rajabu Mngoi, kuituhumu Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuwa imeshindwa kufanya usafi, kuimarisha ulinzi na kuboresha miundombinu sokoni hapo, halmashauri imeibuka na kujivua lawama. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Badala yake msemaji wa halmashauri hiyo, David Langa amewalalamilia wadau wa soko kuzembea kuwaripoti waharibifu wa miondombinu sokoni hapo.

Langa ameliambia MwanaHALISIOnline kuwa wauza samaki ndio wanaotakiwa kuwa walinzi wa mazingira ya sokoni na kutoa ushirikiano kwa halmashauri juu ya uharibifu.  

Amesema, “Halmashauri imetoa magari ya kutosha na wasafishaji wa kutosha kwaajili ya usafi wa soko hilo, ila wanaosababisha mazingira kuonekana machafu ni wafanyabiashara wenyewe.

“Usafi unafanyika kila siku ila inategemeana na muda gani? Kwa mfano asubuhi unaweza kukuta ni pasafi na ukipita mchana unakuta pachafu. Swala la ubovu wa mitaro ya maji taka, wafanyabiashara ndio wanaiharibu, tulishawajengea mitaro lakini wanabomoa, sisi hatuwezi kuwakamata ila tunategemea ushirikiano toka kwa wadau wa soko.”

Langa amesema, halmashauri ipo mbioni kumalizia ujenzi wa majiko banifu ambayo hayakuwepo, na kwamba wanajipanga kuboresha miundombinu iliyopo.

Ameongeza kuwa kuanzia 8 Aprili mwaka huu, watafanya sensa upya ili wajue idadi ya wafanyabiashara wa sokoni hapo ili kupata idadi ya walipa ushuru na kuwaondoa wasiohusika.

“Soko lina uwezo wa kubeba wafanyabiashara 200 tu, na ndio hawo waliopo kwenye orodha, lakini sasa kinachoonekana wavamizi wamekuwa wengi,  wanasababisha mrundikano  na hivyo kuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira,” amesema Langa.

error: Content is protected !!