Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Jiji la Arusha yafikia asilimia 60 makusanyo
Habari Mchanganyiko

Jiji la Arusha yafikia asilimia 60 makusanyo

Spread the love

HALMASHAURI ya jiji la Arusha imekusanya asilimia 60 ya mapato yatokanayo na miradi ya ndani ya maendeleo kwa kipindi cha bajeti ya mwaka 2016/17, anaandika Mwandishi Wetu.

Akiwasilisha taarifa mbele ya Baraza la Madiwani kwenye kikao cha robo ya nne cha kufunga mwaka wa bajeti, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji,  Athuman Kihamia, amesema halmashauri hiyo imefanikiwa kukusanya mapato yake kwa asilimia 60 kutoka vyanzo mbalimbali vya miradi ya maendeleo na matumizi ni asilimia 40 ambayo yalitumika kulipa mishahara ya wafanyakazi na kuendesha ofisi.

Amesema ndani ya mwaka wa bajeti wanaweza kupiga hatua kwa kufanya matengenezo ya barabara za lami na changarawe kwa asilimia kubwa, ujenzi na ukarabati wa vyumba vya madarasa 87 kwa shule za msingi na sekondari na vituo vitano vya afya ambavyo vipo katika hatua za mwisho kukamilika.

Wakati huo huo, Baraza hilo limefanya uchaguzi wa Naibu Meya ili aweze kuongoza baraza hilo kwa kipindi kingine cha mwaka mmoja huku madiwani wawili waliogombea nafasi hiyo  ni Abdulrazak Tojo (CCM) ambaye anatoka Kata ya Mjini Kati na aliyekuwa Naibu Meya wa Jiji hilo,  Viola Lekindikoki.

Aidha, baraza hilo limezindua kanuni mpya zitakazotumika kuongoza baraza hilo. Akizindua kanuni hizo, Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro, amesema kanuni hizo ndizo zitakazoongoza madiwani hao kuendesha vikao vyao vya baraza hilo, pia alisisitiza madiwani hao kuzingatia kanuni hizo zilizosomwa na Mwanasheria wa Jiji la Arusha.

Baada ya uzinduzi wa sheria hizo, wenyeviti wa kamati mbalimbali za kudumu waliwasilisha taarifa za kamati zao za ikiwemo Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya, Kamati ya Mipango miji, Mazingira na Ujenzi sanjari na Kamati ya Kudhibiti Ukimwi.

Akiwasilisha taarifa ya ripoti ya kamati ya Uchumi, Afya na Elimu na Diwani wa Kata ya Ngarenaro, Isaya Doita, alisema wamehamasisha kaya 2,157 kufanya ununuzi wa madawati 1, 800 katika shule za msingi.

Huku Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji, Ally Bananga, akiwasilisha ripoti yake, alisema ufinyu wa bajeti kwa mwaka wa Fedha 2016/17 umepelekea baadhi ya maeneo kushindwa kuboresha mazingira, pia mgao wa maji AUWSA unafanya bustani za mizunguuko kutokuwa kijani cha kuvutia ikiwemo kuangalia uwezekano wa kuchimba visima kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

Habari Mchanganyiko

Uholanzi wampongeza Rais Samia kuimarisha vyombo vya habari, demokrasia

Spread the love  UBALOZI wa Uholanzi nchini Tanzania, umempongeza Rais Samia Suluhu...

error: Content is protected !!