
Afisa masoko wa jiji la Dodoma James Yuna akiwaondoa wafanyabiashara wanaopanga biashara zao kwenye maeneo hatarishi ya kiafya katika soko la Sabasaba
JAMES Yuna, Ofisa Masoko wa Jiji la Dodoma, amewataka wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga) kuacha kufanya biashara kwenye maeneo yasiyo rasmi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Ametoa kauli hiyo leo Jumanne, tarehe 2 Februari 2021, wakati akiwaelimisha baadhi ya wafanyabiashara hao waliopanga bidhaa zao sehemu za waenda kwa miguu ikiwemo kwenye madaraja.
Amesema, baadhi ya madaraja hayo yaliyopo ndani ya jiji hilo, yamevamiwa na wamachinga kwa kuweka bidhaa mbalimbali bila kujali maana halisi ya matumizi yaliyokusudiwa na mipango miji.
“Niombe tuheshimu matumizi ya madaraja haya ambayo serikali yameyajenga ili kuwarahisisha watembea kwa miguu kupita sehemu salama, kwa maana hiyo ninahitaji yawe wazi na sivyo vinginevyo,” amesema.
Pia, amewataka mamalishe ndani ya masoko kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya kwa kuweka vyombo vya kunawa na sabuni, ili kujikinga na magonjwa mbalimbali ya maambukizo.
Akizungumza na mama lishe wa Soko Kuu la Majengo, jijini Dodoma amesema, wanatakiwa kuchukua tahadhali ya magonjwa ya maambukizi.
More Stories
Milioni 30 kuhifadhi misitu ya vijiji Morogoro
Bosi Tarura aagiza ujenzi daraja Kaseke, 1.5 milioni zirejeshwe
Operesheni Samia yawapatia vijana 45,047 mafunzo JKT