Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Jeshi Urusi kuokoa wanafunzi wa Tanzania waliokwama Ukraine
Habari za Siasa

Jeshi Urusi kuokoa wanafunzi wa Tanzania waliokwama Ukraine

Spread the love

SERIKALI ya Urusi imetengeneza njia salama ya kuwawezesha wanafunzi raia wa Tanzania wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Sumy kilichopo nchini Ukraine kuvuka na kurejea nchini ili kuepuka mashambulizi ya vita vinavyoendelea kati ya nchi hizo mbili. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo yameelezwa katika taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi jana tarehe 5 Machi, 2022 kupitia mitandao ya kijamii.

Taarifa hiyo imewataka wanafunzi hao kuelekea eneo la Sudja ambako watapokelewa na jeshi la Urusi kuanzia jana.

“Kutoka Sudja watasafirishwa na jeshi hilo hadi eneo la Belgorod ambapo watapokelewa na maofisa wa Ubalozi wa Tanzania uliopo Moscow kwa taratibu zingine za kurejea nyumbani Tanzania.

“Wanafunzi wanashauriwa kutoka chuoni kwa makundi na kubeba bendera ya Tanzania ili kuwatambulisha wanapopita kwenye safe corridor hii ili kurahisisha uratibu wa zoezi la mapokezi. Pia wanahimizwa kuwasiliana na timu ya mapokezo wakifika eneo la Belgorod kupitia namba +79 267 666 228 WhatsApp +255 759 068 937,” imesema taarifa hiyo.

Wanafunzi wa Kitanzania walio katika mji wa Sumy nchini Ukraine wameruhusiwa kutoka nchini humo kupitia mpaka wa Urusi baada ya mazungumzo ya kidiplomasia kufanyika na Serikali ya Urusi kuridhia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!