Monday , 5 June 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Jeshi Sudan: Wamkamata Rais Bashir, kuongoza nchi miaka miwili
KimataifaTangulizi

Jeshi Sudan: Wamkamata Rais Bashir, kuongoza nchi miaka miwili

Ahmed Awad Ibn Auf, Waziri wa Ulinzi wa Sudan
Spread the love

BAADA ya Jeshi la Sudan kumng’oa madarakani Rais wa taifa hilo, Omar al-Bashir, limetangaza hali ya hatari katika kipindi cha miezi mitatu,  huku likisema litaongoza katika kipindi cha miaka miwili mfululizo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Akitangaza uamuzi wa kuing’oa serikali ya Al-Bashir madarakani leo tarehe 11 Aprili 2019 kupitia televisheni ya taifa ya Sudan, Waziri wa Ulinzi Sudan, Ahmed Awad Ibn Auf amesema jeshi la nchi litaongoza katika kipindi cha cha miaka miwili cha mpito.

Ibn Auf amesema al-Bashir amekamatwa na Jeshi na kuwekwa katika sehemu salama, huku mipaka ya taifa hilo ikifungwa.

“Nitangaza kama Waziri wa Ulinzi kung’oa utawala na kumweka kiongozi wake katika sehemu salama,” amesema Ibn Auf.

Waziri huyo wa masuala ya ulinzi nchini Sudan amesema katika kipindi cha miaka miwili cha uongozi wa jeshi, taifa hilo litafanya mchakato wa kurekebisha katiba yake, ili kuandaa mazingira mazuri ya ufanyikaji wa uchaguzi huru na wa haki.

Ibn Auf amesema katika utawala wa jeshi, haki za binadamu zitaheshimiwa.

Hatua hiyo ya Jeshi nchini Sudan kung’oa utawala wa al-Bashir umekuja baada ya maandamano ya amani ya wananchi yaliyofanyika miezi kadhaa, kushinikiza rais huyo aliyedumu madarakani kwa miaka 30 kuachia ngazi.

Baada ya Jeshi kutangaza hatua hiyo, maelfu ya wananchi wa Sudan walitamalaki katika mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum wakjishangilia Al-Bashir kuondolewa madarakani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Miili ya waliofariki kwenye ajali ya treni India, kukabidhiwa baada ya vipimo vya DNA

Spread the love  TAKRIBANI watu 260 wamefariki na wengine karibu 650 wamejeruhiwa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kifo cha mwanafunzi UDOM: Tume yamsafisha naibu waziri

Spread the loveTUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini (THBUB),...

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Kimataifa

Kauli ya Rais wa China kuhusu ajira yawakatisha tamaa vijana

Spread the love  KAULI ya hivi karibuni ya Rais wa China, Xi...

error: Content is protected !!