May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jeshi latangaza kutwaa madaraka Burkina Faso

Spread the love

 

Jeshi nchini Burkina Faso limetangaza kutwaa madaraka baada ya kufanya mapinduzi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Tangazo hilo la jeshi limetolewa kupitia televisheni ya umma jana Jumatatu tarehe 24 Januari, 2022.

Hatua hiyo imekuja saa chache baada ya jeshi hilo kumshikilia Rais Roch Kabore katika mji mkuu Ougadougou, huku likiahidi kufanyia kazi ratiba ya uchaguzi katika siku za baadae.

Wanajeshi walianza kuasi siku ya Jumapili, na kisha Kabore alikamatwa Jumatatu, licha ya kuwaomba wanajeshi hao kuweka chini silaha zao.

Siku ya Jumapili, mamia ya watu walijitokeza kuwaunga mkono wanajeshi hao na baadhi yao walichoma moto makao makuu ya chama tawala. Amri ya kutotoka nje wakati wa usiku imewekwa.

Haijulikani wapi wanamshikilia rais huyo, lakini hakujawa na vurugu za nje.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani mapinduzi hayo huku Umoja wa Ulaya ukitoa wito wa kuachiwa mara moja kwa Kabore.

Jeshi la Burkina Faso linafuata nyayo za utawala wa kijeshi katika taifa jirani la Mali, ambao ulitwaa madaraka mwaka 2020.

error: Content is protected !!