November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jeshi la Uhamiaji: Tumejipanga kuelekea 2022

Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Dk. Anna Makakala

Spread the love

 

JESHI la Uhamiaji nchini Tanzania, limesema limejipanga kutoa huduma bora kwa wananchi, pamoja na kudhibiti matukio ya uhamiaji kinyume cha sheria, katika mwaka mpya wa 2022. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano, tarehe 29 Desemba 2021, jijini Dar es Salaam na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, akiwavalisha nishani za miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara, maafisa wa jeshi hilo, kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan.

“Kuelekea mwaka mwingine mpya wa 2022, tumejipanga kuonyesha sisi ni jeshi tuko timamu. Kwanza, kuongeza ubora wa huduma ambazo tunatoa kwa wananchi na wageni wote, kutoka nchi mbalimbali. Maana yake sisi ni wadau katika kukuza uchumi kupitia utalii na wawekezaji wanaokuja Tanzania,” amesema Dk. Makakala.

Dk. Makakala amesema “pili, kushirikiana na majeshi mengine kuongeza ulinzi wa nchi yetu, katika mipaka yote na ndani ya nchi. Kuhakikisha tunapambana na wahamiaji haramu, tunafanya kazi karibu na wananchi. Tunawaomba wawe karibu nasi na kutoa taarifa zozote zile ambazo wanaona kuna watu ambao hawaeleweki.”

Akizungumzia zoezi la uvalishaji nishani maafisa wa uhamiaji, Dk. Makakala amesema, limewaongezea motisha ya kufanya kazi.
“Leo ni siku ya kihistoria kwa Jeshi la Uhamiaji, kwa mara ya kwanza tangu kupata uhuru askari, maafisa uhamiaji wanapata nishani kutoka kwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu. Maafisa wamepata mori na motisha, kuona kweli na wao mchango wao unatambulika,” amesema Dk. Makakala.

Tanzania Bara ilipata uhuru wake kutoka Waingereza, tarehe 9 Desemba 1964, ambapo tarehe 9 Desemba mwaka huu, ilitimiza miaka 60 uhuru.

error: Content is protected !!