May 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Jeshi la Tanzania lataka wananchi waishio porini kuondoka

Moja ya misitu iliyopo Tanzania

Spread the love

JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limewataka raia kuondoka porini karibu na mpaka wake na taifa la Msumbiji, wakati huu wanapojiandaa kupambana na wanamgambo waliojipachika jina la “wapiganaji wa kiislamu.” Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mkuu wa operesheni hiyo alisema, jeshi litaanza kuwatafuta wahalifu katika pori la Ruvuma, na baadaye Mtwara na Lindi.

Taarifa kwamba serikali ya Tanzania imepanga kutumia majeshi yake kufanya “operesheni maalum” katika mpaka wake na Msumbiji, zinakuja katika kipindi ambacho serikali ya Marekani imetahadharisha kuwapo makundi ya kihalifu katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wanamgambo hao wanafanya operesheni zao eneo la Kaskazini la Msumbiji, liitwalo Cabo Delgado, huku wakiungwa mkono na wanamgambo wa Islamic State.

Mkuu wa operesheni maalum ya Marekani barani Afrika, Meja Jenerali Dagvin Anderson, amewaambia waandishi wa habari kuwa kundi hilo limekuwa likipata msaada kutoka nje, hali inayolifanya kuwa hatari zaidi.

Wanamgambo hao wanadaiwa kushambulia vijiji mbalimbali katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Alisema, “tumewashuhudia katika kipindi cha miezi 12 mpaka 18 wakiimarisha uwezo wao wa mashambulizi, na kutumia mbinu ambazo hutumika pia katika maeneo mengine ya ulimwengu, hasa Mashariki ya Kati ambako kuna makundi yenye uhusiano na Islamic State.”

Uasi wa wanamgambo wa kiislamu waliojitokeza katika kona ya mbali za Msumbiji umegeuka kuwa vita vya wazi katika wiki za hivi karibuni.

Ripoti za mauaji ya watu, kukatwa kichwa na kutekwa nyara kwa miji miwili katika mkoa wa Cabo Delgado, ni vitendo ambavyo vimekuwa vikiripotiwa kila siku, aliandika mwandishi wa BBC Africa, Andrew Harding.

Me mwaka huu, Tanzania ilipeleka majeshi yake katika mikoa hiyo ya mpakani baada ya kuibuka kwa shambulio la lililotekelezwa na wapiganaji wa kiislamu.

Taarifa zinasema, wapiganaji hao tayari wamevamia miji kadhaa na kuua mamia ya watu na maelfu kuhama makazi yao.

Picha za video, zilizopigwa Aprili mwaka huu kwa simu ya mkononi, wilayani Muidumbe zilikuwa ni ushahidi wenye nguvu kuwa mzozo uliokuwa gizani katika eneo hilo la Kaskazini mwa taifa hilo la Kusini Mashariki mwa AfrikaMsumbiji.

Aidha, picha nyingine za video zilizopigwa katika eneo la bandari Mocimboa da Praia, ambalo lilidhibitiwa kwa muda na wanamgambo tarehe 24 Machi, zinaonyesha wanamgambo hao walidhibiti mji mwingine muhimu wa Quissanga.

‘’Sasa wana silaha na magari, yanayowafanya waweze kutembea kirahisi na kufanya mashambulizi kwenye eneo kubwa. Na hutumia sare za wanajeshi. Hivyo, watu huchanganyikiwa na kuogopa,” anasema Askofu wa kikatoliki wa Pemba, Luiz Fernando Lisboa.

error: Content is protected !!