Tuesday , 26 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Jeshi la Sudan lasitisha mazungumzo na wanamgambo wa RSF
KimataifaMakala & Uchambuzi

Jeshi la Sudan lasitisha mazungumzo na wanamgambo wa RSF

Jenerali Mohamed Hamdan Daglo
Spread the love

 

JESHI rasmi la serikali ya Sudan, limesitisha ushiriki wake katika mazungumzo ya kusimamisha mapigano kati yake na wanamgambo wa Rapid Support Forces RSF yaliyosimamiwa na Marekani na Saudi Arabia. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza kwa sharti la kutotambulishwa jina lake, afisa wa serikali aliyezungumza na shirika la habari la AFP, alieleza kuwa jeshi la serikali lilichukuwa uamuzi huo kutokana na wanamgambo hao, kutotekeleza makubaliano ya kusitisha mapigano.

“Kundi la RSF halijawahi kutekeleza hata sharti moja la mkataba huo wa muda mfupi wa kusitisha mapigano, ambao uliwaelekeza kuondoa vikosi vyao katika hospitali na majengo ya makazi, na kwamba mara kwa mara, wamekuwa wakivunja mkataba huu,” ameeleza afisa huyo.

Alisema, “jeshi limechukua uamuzi huo, kwa sababu waasi hawajawahi kutekeleza hata kipengele kimoja cha usitishaji mapigano kwa muda mfupi.”

Chanzo cha kidiplomasia cha Sudan pia kililifahamisha shirika la habari la Reuters kuhusu kujiondoa kwa jeshi katika mazungumzo tete ya kusitisha mapigano, ambayo yanalenga kuwezesha upatikanaji wa misaada ya kibinadamu.

Siku ya Jumatatu, wapatanishi kutoka Marekani na Saudi Arabia walisema jeshi na RSF walikubaliana kuongeza muda wa usitishaji mapigano kwa ajili ya kutoa fursa ya msaada wa kibinadamu kwa siku tano.

Hata hivyo, mapigano yaliendelea katika maeneo kadhaa ya Sudan, ikiwa ni pamoja na mji mkuu, Khartoum, ambapo RSF ilisema ngome yake imeshambuliwa.

Jeshi lilisema kuwa limezuia shambulio la RSF kwenye mji wa kati wa El-Obeid.

Unaweza pia kusoma: Haya yanajiri siku mbili baada ya Marekani na Saudi Arabia, kueleza kuwa jeshi la serikali na wanamgambo wa RSF, walikuwa wamekubaliana kuongeza kwa siku tano muda wa mkataba wa msaada wa kibinadamu ambao ulikiukwa mara kwa mara katika wiki iliyotangulia.

Hata hivyo, pamoja na kuwapo kwa ahadi hizo, mapigano yalizuka tena jana Jumanne jioni katika maeneo ya Khartoum na eneo la magharibi mwa mji wa Darfur.

Wakati wa ziara ya kutembelea wanajeshi wake katika mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum, jana Jumanne, tarehe 30 Mei 2013, kiongozi wa jeshi la serikali Abdel Fattah al- Burhan, alisema kuwa jeshi liko tayari kupigana hadi kupata ushindi.

Kikosi cha wanamgambo cha RSF kinaongozwa na aliyekuwa Naibu Kiongozi wa Burhan ambaye sasa ni hasimu wake mkubwa, Jenerali Mohamed Hamdan Daglo.

Jenerali Burhan alimfurusha mamlakani jenerali mwenzake huyo, siku chake baada ya kuanza mapigano.

Chanzo cha taarifa kutoka kambi ya Jenerali Daglo kinasema, kitatekeleza haki yake ya kujilinda na kulishtumu jeshi la serikali kwa kukiuka mkataba.

Katika taarifa yake ya jana Jumanne, RSF ilisema kuwa imejitolea katika mkataba wa kusitisha mapigano, licha ya ukiukaji wa mara kwa mara kutoka upande wa jeshi la serikali.

Mkataba huo wa kusitisha mapigano unafuatiliwa kwa karibu na Marekani na Saudi Arabia ambazo zinasema, umekiukwa na pande zote mbili, lakini umeruhusu utoaji msaada kwa takriban watu milioni mbili.

Wakati hayo yakiendelea, Umoja wa Mataifa (UN), baadhi ya mashirika ya misaada, balozi na sehemu ya serikali kuu ya Sudan, zimehamisha shughuli zao hadi katika bandari ya Sudan, ambayo ni kitovu kikuu cha usafirishaji katika bahari ya Shamu ambako kumeshuhudia misukosuko michache.

Kulingana na mradi unaochunguza maeneo ya mizozo ya kivita, tangu mapigano kuzuka kati ya makundi hayo pinzani, 15 Aprili mwaka huu, zaidi ya watu 1,800 (elfu moja na mia nane) wameuawa.

UN wanasema, zaidi ya watu milioni moja wamepoteza makazi na takribani 350,000 wametoroka nchi hiyo kuelekea ng’ambo ikiwa ni pamoja na zaidi ya watu 170,000 waliokimbilia Misri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Uvamizi wa kijeshi Milango ya bahari ya Taiwan G7 yapinga China

Spread the loveMKUTANO wa Mawaziri wa Mambo ya nje wa nchi za...

Kimataifa

Rais Kagame kuwania muhula wa nne

Spread the loveRais wa Rwanda, Paul Kagame amesema atawania muhula wa nne...

Kimataifa

Ukraine kufungua kituo cha nafaka Kenya

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto amesema serikali ya Ukraine inapanga...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Prof Mwafenga ulijiamini katika utendaji wako na degree zako 10 – Maige

Spread the loveKIFO cha Prof Hadley Mpoki Mwafenga- Afisa Usimamizi wa Fedha...

error: Content is protected !!