August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jeshi la Polisi linajifedhehesha

Spread the love

AKIZUNGUMZA wakati wa kupokea ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015, Rais John Magufuli alisema siasa kwa sasa hazina nafasi hadi baada ya miaka mitano, anaandika Josephat Isango.

Kwa maneno yake bila kushurutishwa, Magufuli alisikika akisema, “niwaombe wanasiasa wenzangu, tufanye siasa za ushindani kwa nguvu zote baada ya miaka mitano ili wananchi watuhoji tuliyoyaahidi, tuliyotekeleza au ambayo hatukutekeleza.”

Kujifedhehesha kunakotajwa kwa jeshi hilo kunatokana kitendo cha kumzuia Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe kufanya mikutano ya ndani na kufungua matawi Jijini Mwanza.

“Kama ilikuwa haramu kwa Mbowe kufanya mikutano ya ndani kwenye matawi ya Chadema mkoani Mwanza na haramu pia kwa Zitto kufanya mkutano wa ndani Dar es Salaam kujadili bajeti, inakuwaje halali kwa CCM kufanya mkutano utakaokuwa na watu zaidi ya 3,000 mjini Dodoma.” Amesema Shaban Selema, mkazi wa Makiungu mkoani Singida

Aliongeza kuwa Polisi wanaonekana wana hila, wanasababisha fujo nchini, wanakandamiza demokrasia na katika mvutano huu, jeshi linaweza kuwa chanzo cha machafuko ya kisiasa.

Inashangaza mwishoni mwa wiki jeshi hilo likaibuka  na kutoa taarifa kwamba halijazuia mikutano  ya kiutedaji ya chama, lakini hatua hiyo ni ‘janja’ ya kukipendelea chama tawala, CCM.

Kama ilikuwa marufuku huko ndani watu kukaa  kwenye mahafali, CCM wanapate uhalali wa kukusanyika tena wengi kuliko wa Chaso, bado jeshi la polisi liseme mkusanyiko huu  ni halali kinyume na agizo la rais?

Jeshi hili kwa sasa limedhihirisha kuwa ni mdau wa shaka kabisa kulea demokrasia na haki nchini. Limejiweka wazi kuwa linamilikiwa na chama cha siasa na linafanya kazi za chama.

Makala zaidi soma gazeti la MwanaHALISI la leo (Julai 11)

 

error: Content is protected !!