January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jeshi la Polisi lawakamata Panya Road 1508

Washiriki wa kundi la Panya Road

Spread the love

UPDATE: 17:15

KAMISHNA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova kwa kushirikiana na Makamanda wa kipolisi wa mikoa ya Ilala, Kinondoni na Temeke wamefanikiwa kuwakamata vijana 1508 wanaofanya uhalifu wa makundi maarufu kama “panya road”, anaripoti Sarafina Lidwino.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Kova alisema msako huo ulioanza Januari 3, 2015 hadi sasa wemeshawakamata watuhumiwa hao ambao wanatokana na makosa mbalimbali yakiwemo upigaji debe, wavuta bangi, ukahaba, mirungi na kamari.

Kova alisema watuhumiwa 959 kati ya hao 1508, tayari wamefikishwa katika mahakama mbalimbali jijini Dar es Salaam, huku 430 wameachiwa kwa dhamana na 119 wameachiwa huru baada ya kutokuwa na hatia.

Alisema watuhumiwa wengine walioachiwa huru kutokana na kutokuwa na ushahidiwa kuhusika na matukio hayo ya ‘panya road’, lakini pia Jeshi la polisi litakuwa nyuma yao ili kuweza kufatilia nyendo zao.

HABARI YA AWALI

KAMISHNA wa Polisi, Kanda Maalum, Dar es Salaam, Suleiman Kova, amedai kuwa jeshi hilo limewakamata viongozi watatu wa kundi la uhalifu la “Panya Road.”

Waliokamatwa, ni Halfan Nurdini (24) na Said Mohamed (22), ambao ni wakazi wa Tandale; na Mohamed Nangula (19), mkazi wa Mburahati kwa Jongo. Anaripoti Sarafina Lidwino.

Kamanda Kova amesema, jeshi lake limejiridhisha kuwa watuhumiwa hao watatu ndiyo vinara wa kupanga uhalifu unaonywa na genge hilo.

Mwishoni mwa wiki iliyopota, kundi la Panya Road, lilizusha tafrani kubwa jijini baada ya kuendesha kichapo, uporaji, vitisho na uhalifu wa kila aina.

 

error: Content is protected !!